Picha:Maktaba/REUTERS. |
Rais wa Marekani Donald Trump amesifia fursa za kibiashara barani Afrika Jumatano, akiwaambia viongozi kadhaa wa mataifa ya Kiafrika ana marafiki wengi anbao huenda Afrika "kupata utajiri."
Wakati wa chakula cha mchana na viongozi kati ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Trump alisisitiza juu ya fursa na changamoto za bara la Afrika.
"Afrika ina uwezo mkubwa wa biashara," alisema. "Nina marafiki wengi sana huenda katika nchi zenu wakijaribu kuwa matajiri, nawashukuru. Wanatumia fedha nyingi," alisema.
"Kwa makampuni ya Marekani ni mahali ambapo wanapaswa kwenda..."
Trump alitangaza kuwa alikuwa akimhamisha balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley kwenda Afrika "kujadili njia za vita na ufumbuzi, na muhimu zaidi, kuzuia."
Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Muhammadu Buhari wa Nigeria walikuwa miongoni mwa viongozi walioshiriki chakula hicho cha mchana.
CHANZO:
thecitizen.co.tz
Comments
Post a Comment