Picha za zinazo onesha kasisi wa Uganda akipigwa mabusu na wafuasi wake miguuni tayari zimekwisha zua gumzo miongoni mwa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa siku za karibuni.
Mtume Elvis Mbonye, mwenye umri wa miaka 40, wa Zoe Fellowship, Jumapili iliyopita aliandaa tafrija ya chakula cha jioni kwa kiingilio cha takribani dola 185 (185$) kwa tiketi za platinum, dola 210 (210$) kwa tiketi za Gold, dola 135 (135$) kwa tiketi za Silver, na dola 75 (75$) kwa tiketi za kawaida.
Ibada za Mbonye hufanyika siku za Jumanne kinyume na za makanisa mangine za Jumapili au Jumamosi, akisema Mungu alimwambia afanye ibada siku za Jumanne.
Wakati alipoanza kanisa mwaka 2014, Mbonye alikuwa na waumini 100, lakini sasa amefikisha waumini 5,000,
vyombo vya habari vya Uganda vinasema.
Mbonye, kabla ya kuhamishia ibada zake kwenye uwanja wa Rugby wa Kyadondo, alikua anakodisha hoteli ya kifahari ya Kampala kwa gharama sawa na dola 13,500 za kimarekani kila wiki.
Mbonye amekua akituhumiwa na watu mbali mbali kwamba anaabudu mashetani ,kitu ambacho amekua anakataa kabisa.
Watu wengi wamekua wakiona aina ya mavazi ya gharama ambayo anayovaa hayafanani na mtu wa Mungu, lakini Mbonye hafikiri hivyo.
"Ndiyo nilivyo, ukiachana na yote mimi ni mtu nisiependa makuu",
aliliambia gazeti la Observer la Uganda katika mahojiano ya Septemba, 2016.
Mbonye anasema Zoe ni neno la Kiyunani kwa 'maisha ya kimungu' na ushirika huu huwavutia watu kutoka kila aina ya maisha, ikiwa ni pamoja na wachungaji kutoka makanisa mbalimbali.
Yote hii ilianza mwaka 2014 wakati Mbonye alifungua milango kwa watu katika Hotel Triangle huko Kampala ambapo alipanga mikutano ya kila mwaka.
"[Lakini] tulipoanza ibada za Jumanne, mahali ambapo tulianza na watu wapatao 100 kulipata mafuriko kwa haraka tulitafuta sehemu nyingine,"
alisema katika mahojiano na Observer.
Ibada zake za Jumanne zinaanza saa 11 jioni lakini waumini wanawasili kanisai saa 9 alasiri na Mbonye hufika saa 1 usiku kuongoza huduma.
Katika ibada ya Agosti 23, 2016, Mbonye alimaliza kuhubiri saa mbili na nusu usiku kwa kuwaita watu wote wanaoitwa Bruno. Watu watatu walijitokeza na aliwaambia kwa usahihi miezi halisi na tarehe walizozaliwa, kabla ya kuongoza umati huo katika nyimbo za sifa na ibada.
Mbonye ni mshabiki mkubwa wa Arsenal mwenye na anasema anapenda kutazama sinema, hasa za kuchekesha, za kipelelezi na za kutisha.
Mke wake anaitwa Harriet Mbonye, mwanamke wa mfanyabiashara ambaye, kwa kushangaza, hajawahi kuhudhuria ibada yake yoyote.
"Lakini yeye (Harriet) anafuatilia ibada hizo kwenye televisheni nyumbani. Anaweza kuanza kutokea kwenye hadhara lakini nadhani huu si wakati sahihi.
Bwana hakuonesha hiyo, "alisema.
Wao wawili wameoana kwa miaka sita sasa.
Siku za mapumziko utampata Mbonye kwenye Kahawa nzuri ya Afrika huko Lugogo lakini pamoja na walinzi wake ambapo anasema kuwa ni hatua za tahadhari.
Mbonye ana mpango wa kujenga jengo la kudumu kwa huduma zake - si kanisa, anasisitiza.
Mtume Mbonye alizaliwa katika familia ya watoto saba ya Leo na Teddy Ntiru wa Bugolobi, ambayo walifariki mwaka 1990 na 1996, kwa mtiririko huo. Alihudhuria shule ya awalu ya Mbuya, shule ya msingi ya Kiswa, Kigezi College Butobere kwa O-level na Standard High School huko Zana kwa ngazi zake za A-level.
Baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere ambapo alihitimu shahada ya Development Studies mwaka 2004.
CHANZO:
edaily.co.ke
Comments
Post a Comment