Baadhi ya wabunge kutoka mkoa wa pwani waliochaguliwa kwa vyama tanzu chini ya muungano wa NASA wametishia kuuhama muungano huo na kujiunga na chama cha Jubilee.
Wakiwahutubia wanahabari Jumatatu, Septemba 18, wabunge hao waliushutumu muungano huo kwa kuwateua wabunge fulani bila kuwashirikisha.
Wakiongozwa na mbunge wa Msambweni, Suleiman Dor, Wabunge hao waliupinga uteuzi wa seneta wa Bungoma ambaye pia ni kigogo wa NASA kuwa kiongozi wa walio wachache katika bunge la seneti na John Mbadi kama kiongozi ya walio wachache katika bunge kitaifa. Seneta wa Siaya James Orengo atakuwa kaimu wa Wetangula katika bunge la seneti Wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni mbunge wa Lugari Ayub Savula,Robert Mbui wa Wiper na Chris Wamalwa wa Ford Kenya. Wabunge hao wa pwani walilalamika kwa kubaguliwa katika uteuzi huo.
Tishio hilo lilimlazimu Odinga kujitokeza na kuifutilia mbali orodha hiyo akisema kwamba majina ya Mbadi na Wetangula pekee ndiyo yaliwasilishwa bungeni. ‘’Sijui kuihusu orodha hiyo ambayo inasambazwa.Najua kwamba tutakaa na kukubaliana kama kundu la wabunge wa NASA,’’ Raila alinukuliwa na Nation.
CHANZO:
Comments
Post a Comment