Jumatatu,Tarehe 25 September,Jiji la Dubai limeshuhudia jaribio la kwanza la teksi za angani zinazofanana na drone (Helicopter zinazoruka bila rubani) katika kila kinachojulikana kama juhudi za serikali ya Dubai kuongoza kwa uvumbuzi katika dunia ya Kiarabu.
Teksi hizo za angani ni zinatengenezwa na kampuni ya Kijerumani inaojulikana kama Volocopter.
Chombo hicho chenye na uwezo wa kubeba watu wawili na muonekano wa mapanga (propeller) 18, kilijaribiwa kwa mara ya kwanza katika hafla maalum iliyondaliwa na mtawala wa Dubai, Sheikh Hamdan bin Mohamed.
Kikiwa kimetengenezwa kwa kufanya safari zisizozidi za dakika 30 , kifaa hicho kimewekewa vitu vingi vya dharura kuhakikisha usalam wa abiuria kama betri za ziada na maparashuti.
Kampuni ya Volocopter inashindana na makampuni zaidi ya kumi yenye uwezo mkubwa kiuchumi kutoka Ulaya na Marekani katika kubuni aina mpya ya usafiri wa mijini.
Miongoni mwa kampuni hizo ni kampuni kubwa ya kutengeneza ndege na vifaa vya angani ya Marekani, Airbus,ambayo imepanga kutengeneza teksi za angani ambazo zitakua zikiendeshwa na mteja mwenyewe itakapofika mwaka 2020.
Katika zoezi hilo linalofadhiliwa na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Google kutengeneza kifaa kitachoitwa "Kitty Hawk" ,Kampuni ya Airbus inashirikiana pia na Uber.
Tazama Video hapa:
CHANZO:
dailymail.co.uk
Comments
Post a Comment