Akizungumza kuhusu habari ya kwamba mkosoaji mkubwa wa serikari ya Tanzania ,Tundu Lissu kupigwa risasi kwenye makao makuu ya Tanzania, Dodoma,Sarah Jackson ambae ni mkurugenzi wa Amnesty International kanda ya Afrika Mashariki ,pembe ya Afrika na nchi za maziwa makuu, Amesema;
" Hili shambulio la woga kwa mmoja wa wanasiasa washindani na maarufu linaamsha wasiwasi juu ya usalama wa sauti za wapinzani nchini (Tanzania), katika majira ambayo nafasi ya kutoa maoni inazidi kusinyaa"
"Mamlaka lazima iwahakikishie Watanzania ulimwengu kwamba shambulio hili halikuhamasishwa na siasa"
"Uhalifu huu usiofaa haupaswi kufagiliwa chini ya zulia, mamlaka za Tanzania lazima zianze uchunguzi makini na wa usawa mara moja kuhakikisha wale waliohusika wanashikiliwa."
AWALI:
Tundu Lissu, ambaye pia anaongoza chama cha wanasheria, Tanganyika Law Society, ni mkosoaji na mshamuliaji mkali wa Rais John Pombe Magufuli.
Alikamatwa Julai kwa kumwita rais dikteta, na tena mwezi Agosti kwa kusema serikali ya Canada inaishikilia ndege iliyonunuliwa na serikali ya Tanzania kwa deni la $ 38m kutoka kwa kampuni ya Canada.
Kwa jumla, amekamatwa mara sita mwaka huu.
CHANZO:
amnesty.org
Comments
Post a Comment