Skip to main content

UNDANI WA MAUAJI YA KUTISHA KWA WAISLAM NCHINI MYANMAR (BURMA).



Waziri Mkuu wa India Narendra Modi anakabiliwa na swala zito la Waislam wa Rohingya ambao wamekimbilia India baada ya kutokea mauaji ya kinyama dhidi yao nchini Myanmar.
Vyanzo vya habari nchini Myanmar vinaeleza kuwa Waislam wa nchi hiyo wamekuwa wakikimbia kuelekea India na Bangladesh.
Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, helikopta za kijeshi zimeendelea kupiga risasi maeneo ya Waislam.
Ripoti hiyo pia inasema kuwa kwa miaka 10 iliyopita, Jeshi la nchi hiyo limekuwa likiwatafuta watu wazima wa jamii hiyo ya Waislam na kuwaua na ndiyo sababu watu wa Rohingya wanakimbilia Bangladesh. Hata hivyo serikali ya Myanmar imekanusha tuhuma hizo dhidi ya Jeshi lake.
Kwa mujibu wa ripoti ya taasisi zinazoshughulikia wakimbizi zikifanya kazi na Umoja wa Mataifa, kiasi cha Waislam wa Rohingya 400 waliuawa wakati wa machafuko hayo na wakati upelelezi ukifanywa na Jeshi.
Kufuatia mauaji hayo Takriban Waislam 40,000 wameondoka kutoka katika makazi yao huko Myanmar na sasa wanapata hifadhi katika majimbo ya Hyderabad, Jammu, Delhi, West Bengal, Uttar Pradesh, Punjab na Rajasthan nchini India.
Masiku machache yaliyopita, Waziri wa Nchi wa India (Mambo ya Ndani ) Kiren Rijiju alisema kuwa Waislam wote wa Rohingya wanaoishi India wataondolewa kurejeshwa makwao. Tangazo hili la serikali linatathminiwa kufuatia ziara ya Waziri Mkuu wa India nchini Myanmar.
Viongozi wa Waislam wa Rohingya wameiomba Mahakama ya Juu kutowarejesha Waislam waliokimbilia India kutokana na sababu ya haki za kibinadamu. Hivi sasa, Mahakama ya Juu imeiambia serikali kuweka wazi msimamo wake juu ya swala hilo.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari ulimwenguni, mauaji haya dhidi ya Waislam wa Rohingya sio kitu kipya huko Myanmar—ambapo siku za nyuma ilikuwa inajulikana kama Burma.
Lakini tukio hili la karibuni limekuza mgogoro huo nakuleta wasiwasi mkubwa juu ya usalama wa Waislam hao.
Mnamo Agosti 25, wapiganaji wachache wa Rohingya walishambulia dazeni ya vituo vya polisi na kambi za kijeshi nchini Myanmar. Kikundi cha wapiganaji kinachojiita Arakan Rohingya Salvation Army kilidai kuhusika na mashambulizi hayo.
Kufuatia upelelezi uliofanyika, Jeshi la nchi hiyo liliunguza nyumba 2,600 za Waislam wa Rohingya jambo ambalo limefanya zaidi ya Waislam 125,000 kukimbilia Bangladesh kuokoa maisha yao.
Inaelezwa kuwa Waislam wa Rohingya wanakandamizwa kuliko jamii yoyote duniani.
Myanmar ni taifa la watu walio wengi wenye kufuata madhehebu ya Buda
Takriban Waislam wa Rohingya milioni 1 wanaishi katika jimbo la Rakhine huko Myanmar.
Waislam hawa wanasadikiwa kuwa ni wakimbizi kutoka Bangladesh na ndio sababu serikali ya Myanmar haiwatambui kama raia wa nchi hiyo.

CHANZO:

Comments

Habari Nyingine Kutoka Kioo17 Swahili;

ORODHA YA NCHI 80 AMBAZO MTANZANIA ANARUHUSIWA KUINGIA BILA VIZA.

         Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza . Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza za kusafiria kama ilivyokuwa nchi za afrika Mashariki. Mhandisi Massauni amebainisha hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo kupitia tiketi ya CCM Rashid Shangazi aliyetaka kujua ni nchi ngapi ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza (viza on arrival). "Zipo nchi 16 kwa Afrika ambazo watanzania wanaweza kuzitembelea bila ya kuwa na viza na duniani zipo 67" alisema Masauni. Aidha Massauni amezitaja nchi hizo kuwa ni Benin, Burkina Faso, Cape Verde, Ivory Coast, Djibouti, Gabon, Gambia, Guinea, Guinea­Bissau, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Sierra Leone pamoja na Togo. Pamoja na hayo Masauni amesema...

PAPA ANAFIKIRIA KURUHUSU WATU WALIOFUNGA NDOA KUTUMIKIA KANISA KAMA MAKUHANI.

Papa Francis anafikiria mipango ya kuruhusu wanaume walio katika ndoa kutumikia kanisa kama makuhani Wakatoliki katika maeneo ya mbali ambapo kuna uhaba wa muda mrefu wa huduma za kiroho. Mpango huo unazingatia mapendekezo yaliyotolewa na maaskofu huko Brazili ambao wanalalamika maeneo fulani wanasimamiwa na kuhani mara kadhaa tu kwa mwaka. Chini ya mapendekezo hayo, watu walio kwenye ndoa wenye imani iliyoidhinishwa, inayojulikana kama 'viri probati' na kanisa, wataweza kujiunga na ukuhani. Mpango unaozingatiwa na Vatican hautaruhusu makuhani waliopo kufunga ndoa, ingawa baadhi ya makuhani wa zamani ambao waliondoka kwenye ukuhani kuanza familia wanaweza kuruhusiwa kurudi. Wanasolojia wanaamini kwamba suala la makuhani walio kwenye ndoa linaweza kukubalika kama sheria ya kutokufunga ndoa litachukuliwa kama suala la nidhamu ya kanisa badala ya sheria. Papa Francis haamini kuondoa sheria ya kutokuoa kwa makuhani waliopo itasaidia kutatu...

KIONGOZI MKUU WA UPINZANI NCHINI ZIMBABWE, MORGAN TSVANGIRAI AMEFARIKI DUNIA.

Kiongozi wa upinzani wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika Kusini, afisa mkuu wa chama chake cha MDC amesema. Bw Tsvangirai, mwenye umri wa miaka 65, aliyekuwa waziri mkuu, alilipotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na saratani ya koloni. "Amefariki jioni hii, familia yake imenitaarifu"  Makamu wa Rais wa MDC, Elias Mudzuri aliliambia shirika la habari la Uingereza, Reuters. Morgan Tsvangirai alizaliwa mnamo Machi 10, 1952 huko Gutu, Zimbabwe. Baba yake alikuwa mfanyakazi wa mgodi, fundi, na mkulima. Alihudhuria Shule ya Msingi ya Guco ya St. Marks. Kisha alihamishiwa Shule ya Msingi ya Chikara Gutu. Kwa elimu yake ya sekondari, alihudhuria Shule ya High Gokomere. Alikuwa waziri mkuu katika serikali ya mseto ya Zimbabwe tangu 2009 hadi 2013. Katika kazi yake ya awali alionekana kuwa mfanyakazi mwenye bidii sana na alifanya kazi katika mgodi wa madini ya nickel( kwa zaidi ya muongo mmoja. Alipanda cheo haraka kutambuliwa na akain...

MWANAMKE WA MIAKA 64 ALIYETAPELIWA $100,000 NA MPENZI ALIYEKUTANA NAE FACEBOOK.

PATRICIA MEISTER (64). Mwanamke mwenye umri wa miaka 64 amesimulia juu ya jinsi alivyotapeliwa dola 100,000 baada ya kupendana na mtu ambaye ambaye hawakuwahi  kukutana . Patricia Meister, kutoka Queensland, Australia alianza uhusiano wa mtandaoni na mtu ambaye alidhani alikuwa mfanyabiashara mwenye umri wa miaka katikati baada ya mtu huyo kumtumiaa ombi la rafiki kwenye Facebook mwaka 2015. Akizungumza na Daily Mail Australia, mwanamke huyo alifafanua wakati alipopiga kichwa juu ya visigino kwa upendo, kabla ya kugundua mpenzi wake wa Italia aitwaye 'Carlos' alikuwa tapeli wa Nigeria. Bi Meister alisema mwanamume huyo alionekana kujali na kufuatilia kila kitu cha maisha yake alipokua anapiga simu kila siku. 'Sijawahi kuwa kwenye tovuti za marafiki(dating websites), na nilokua natumia Facebook kwasababu za kibiashara. Kwa hiyo nilipopata ombi la urafiki, nilidhani haiwezi kuwa na madhara yoyote ", Alisema. 'Nadhani wakati ule, nilikua ...

UGANDA IMEWAFUKUZA WATAALAM WA KIJESHI KUTOKA KOREA YA KASKAZINI.

Uganda imefukuza wataalamu wa kijeshi wa Korea Kaskazini na wawakilishi wa makampuni ya Kaskazini ya Korea, ikiwa ni pamoja na mfanyabiashara wake mkubwa wa silaha za juu kutokana na mataifa ya Kiafrika kukabiliwa na shinikizo la kuzingatia vikwazo vya Umoja wa Mataifa(UN) juu ya mpango wa silaha za nyuklia wa Pyongyang. "Raia wa Korea ya Kaskazini waliobaki katika taifa hilo la Afrika Mashariki ni wanadiplomasia na watu binafsi tu ", Okello Oryem, naibu waziri wa mambo ya kigeni, aliiambia The Associated Press. "Tunafuatana kabisa," alisema Oryem, akiongezea kwamba Uganda ina uhusiano wa kawaida wa kidiplomasia na Korea Kaskazini. Uganda hasa ilidai kuondoka kwa watu wanaowakilisha Shirika la Biashara la Maendeleo ya Madini ya Korea. Ni mkataba wa msingi wa Korea Kaskazini na chini ya vikwazo vya U.N. na U.S. Uhamisho huo unaashiria mabadiliko ya sera kwa serikali ya Uganda, ambayo hapo awali ilikuwa na mahusiano ya mazuri na Pyongyang. Korea ya Kaska...

BAYERN MUNICH WANAJENGA VYUMBA VYA HOTELI NDANI YA UWANJA.

Huu ndio utakaokuwa muonekano wa vyumba hivyo kwa ndani. Picha: Mariot International. Kama sehemu ya mpango wa miaka mingi ya Bayern na  kampuni kubwa ya hoteli za Mariot na Courtyard, mashabiki hivi karibuni wataweza kupata fursa ya kukaa katika vyumba ambavyo vina dirisha linaloangalia uwanja wa Alianz Arena moja kwa moja. Vyumba hivyo vya kifahari vya kulala vitakuwa na kitanda cha kikubwa na seti ya televisheni - tu ikiwa umechoka na hat-trick za Robert Lewandowski. Pia kutakuwa na mahali pa moto ambayo ni maalumu kwa siku za mechi kwenye majira ya baridi. Mkurugenzi Mtendaji wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge alisema: "Tunafurahia bidhaa mbili zinazoongoza kama hoteli Courtyard zinazomilikiwa na kampuni ya Marriott na FC Bayern kuingia katika ushirikiano huu wa muda mrefu kibiashara. "Tunapendezwa na bidhaa mbili zinazoongoza kama Courtyard na Marriott na FC Bayern kuingia katika ushirikiano wa muda mrefu," "Kutokana na kwamba Marri...

AMNESTY INTERNATIONAL YAIONYA SERIKARI YA TANZANIA.

Akizungumza kuhusu habari ya kwamba mkosoaji mkubwa wa serikari ya Tanzania ,Tundu Lissu kupigwa risasi kwenye makao makuu ya Tanzania, Dodoma, Sarah Jackson ambae ni mkurugenzi wa Amnesty International kanda ya Afrika Mashariki ,pembe ya Afrika na nchi za maziwa makuu, Amesema; " Hili shambulio la woga kwa mmoja wa wanasiasa washindani na maarufu linaamsha wasiwasi juu ya usalama wa sauti za wapinzani nchini (Tanzania), katika majira ambayo nafasi ya kutoa maoni inazidi kusinyaa" "Mamlaka lazima iwahakikishie Watanzania ulimwengu kwamba shambulio hili halikuhamasishwa na siasa" "Uhalifu huu usiofaa haupaswi kufagiliwa chini ya zulia, mamlaka za Tanzania lazima zianze uchunguzi makini na wa usawa mara moja kuhakikisha wale waliohusika wanashikiliwa." AWALI: Tundu Lissu, ambaye pia anaongoza chama cha wanasheria, Tanganyika Law Society, ni mkosoaji na mshamuliaji mkali wa Rais John Pombe Magufuli. Alikamatwa Julai kwa kumwita rais diktet...