Image: AFP. |
Ni nini kinachotokea unapoweka majogoo mawili katika banda moja? Amani haitadumu.Hii ndio kilichotokea katika klabu ya PSG.
Tayari kuna idadi kubwa ya matukio ya kutoelewana kati ya Neymar na Cavani, lakini sasa inaonekana kwamba mpasuko huo haujaishia uwanjani.
Neymar ameacha kumfuatilia Cavani kwenye Instagram baada ya tukio kati ya wachezaji hao wawili katika mechi ya mwisho ya ligi kuu ya Ufaransa. Katika mechi hiyo Cavani alionekana kumkatalia Neymar kupiga penati na wakaonekana kubishana juu ya hilo.
"Ney" aliondoka Barcelona kwa sababu hakutaka kuwa kwenye kivuli cha Messi. Alitaka kuwa nyota hivyo alijiunga na PSG, lakini sasa anacheza pamoja na Cavani, ambaye jitihada zake kuwa mchezaji bora wa Ligue 1 haziwezi kumruhusu Neymar kupewa jukumu la kupiga penati na free kick. Cha kushangaza na kuchekesha ni kwamba Messi alikuwa tayari kutoa ruhusa hizo kwa Neymar walipokua Barcelona.
Sasa, Emery atapaswa kukabiliana na vita hivyo vya mafahari na tayari ameonya kuwa ataingilia kati ikiwa wote wawili wanaendelea kuendelea kubishana na kutokuangaliana machoni. Inaonekana kama watahitaji kufanya kazi kidogo kwenye uhusiano wao.
CHANZO:
besoccer.com
Comments
Post a Comment