Zaidi ya ng’ombe 4000 kutoka Tanzania wanashikiliwa katika kaunti ya Kajiado na Wamasai wa Kenya baada ya kuingizwa kutoka Tanzania.Hata hivyo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina alisema wakati akizungumzia suala hilo kuwa Serikali haina taarifa ya kuchukuliwa kwa ng’ombe hao na akasisitiza Hali hii imekuja wiki mbili baada ya Serikali ya Tanzania kukamata ng’ombe 1,305 katika Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa kosa la kuingizwa kinyume na utaratibu.
Kwa mujibu wa kipindi cha Dira ya Dunia, kinachorushwa na BBC, wafugaji wa eneo lililopo kusini mwa Kenya wanaonekana kuendeleza kisasi, viongozi wanafanya juhudi za kuzuia ukamataji wa mifugo.
Kamishna wa eneo hilo Harsama Kello aliliambia Shirika la BBC kuwa anaendelea na jitihada za kuzuia ukamataji wa mifugo kutoka Tanzania kwa kuwa hali hiyo inaharibu taswira ya nchi hizi mbili jirani.
“Wafugaji wamepanga kunyang’anya mifugo yote itakayoingia kutoka Tanzania kwenda Kenya. Najaribu kwa nguvu zangu zote kuizuia jambo hili" , alisema Kello.
“Hakuna namna tunaweza kuruhusu suala hili kuendelea. Ni hatua mbaya kwa diplomasia na uhusiano wa nchi jirani na tunashirikiana kwa mambo mengi,” alisema.
Wamasai wa eneo hilo wamekuwa wakivuka mipaka kwa ajili ya kutafuta malisho kutokana na kukosa maeneo ya kutosha ya kulisha mifugo.
Kuna uhaba kutokana na mmomomyoko wa udongo, migogoro kati ya wakulima na wafugaji na kuwa na mifugo mingi.
CHANZO:
Comments
Post a Comment