Serikali ya Emmerson Mnangagwa inataka kutumia huduma za Interpol(Polisi wa kimataifa) kuwasaka washirika wa karibu wa rais Robert Mugabe ambao walikimbia nchi wakati jeshi lilipositisha utawala wa zamani mwezi uliopita.
Mawaziri wa zamani Jonathan Moyo, Saviour Kasukuwere na Paddy Zhanda wanaaminika kuwa ndio walengwa wakuu wa msako huo kwa sababu za tuhuma za uhalifu unaohusishwa na rushwa.
Tume ya kupambana na rushwa ya Zimbabwe, Zimbabwe Anti-Corruption Commission (ZACC) inachunguza tuhuma za Moyo za wizi katika Shirika la Maendeleo ya Wanawake wa Zimbabwe wakati wa utawala wa Mugabe. Moyo alidai kuwa Mnangagwa alikuwa akitumia ZACC kutekeleza visasi binafsi vinavyohusishwa na mapambano ya kutaka kumrithi Mugabe.
ZACC tayari imekamata washirika wa karibu wa Mugabe yaani Joseph Made, Walter Chidakwa, Ignatius Chombo na Jason Machaya. Viongozi wa zamani wa vijana wa chama tawala cha Zanu PF, Kudzanai Chipanga na Innocent Hamandishe pia walikamatwa kwa mashtaka ya jinai wakati jeshi lilipokua linachukua utawala.
Waziri wa Mambo ya Ndani Obert Mpofu alithibitisha katika mahojiano na gazeti la 'The Standard' la Zimbabwe, kwamba serikali itatumia Interpol kuwasaka wale walio nje ya nchi.
"Tunafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha kuwa wale waliofanya uhalifu ndani ya Zimbabwe ambao wako nje ya Zimbabwe wanaletwa. Ikiwa inamaanisha kushirikisha Interpol, "
alisema.
"Mchakato huu ni wa pili, tunaangalia uchunguzi wa ndani na uchunguzi wa nje na uchunguzi wa nje, unahusisha Interpol."
Hata hivyo, Mpofu alikataa kusema kuwa Kasukuwere, Zhanda na Moyo ndio walengwa wakuu ya uchunguzi huo.
"Tunasema juu ya wote waliofanya uhalifu nchini Zimbabwe na ikiwa wamefanya uhalifu, watashiriki katika zoezi hili,"
alisema.
"Kama wale watatu wanahusika katika uhalifu uliofanywa nchini Zimbabwe watakuwa sehemu ya uchunguzi wetu."
Siku ya Ijumaa, Mnangagwa alisema kuwa amewasamehe wafusai wa G40, ikiwa ni pamoja na wale waliokimbia kwenda nchi nyingine, lakini walisema watatu kati yao bado wanatuhuma za kujibu. Lakini hakutaja mtu yeyote kwa jina.
Serikali mapema mwezi huu walifungia akaunti za benki za Kasukuwere na Moyo. Wakati huo huo, pamoja na matangazo ya umma ya Mnangagwa kwamba wa Zimbabwe wanapaswa kuruhusu "maadili kuwa sawa", dalili ni kwamba taasisi za serikali zinatafuta wafuasi wa G40.
Kulingana na ripoti, Chipanga amepoteza shamba lake huko Rusape kama adhabu ya kumsaidia mke wa rais wa zamani ,Grace Mugabe dhidi ya Mnangagwa.
Mkurugenzi wa shirika la haki za binadamu la nchi za kusini mwa Afrika Dewa Mavhinga alisema serikali ya Zimbabwe inapaswa kuthibitisha kuwa kamata kamata hiyo haina nia ya kulipiza kisasi kundi la Zanu PF Lacoste, lililoshinda vita ya kurithi urais wa nchi hiyo kutoka kwa Robert Mugabe.
"Serikali ya Mnangagwa ina changamoto ya kuonyesha kwamba kukamatwa kwa hivi karibuni kwa mawaziri wa zamani hayaendeshwi na kisasi na uwindaji wa mchawi wa kisiasa na kwamba kuna dhamira kamili ya kuondokana na rushwa," alisema.
"Je, serikali itawakamata mawaziri wa sasa ambao wamekuwa wakihukumiwa hadharani kwa vitendo vya rushwa kama Obert Mpofu, ambaye alidaiwa kudai rushwa ya dola milioni 10 za kimarekani kutoka kwa Lovemore Kurotwi?
"Kuna haja ya haraka ya kujenga uaminifu kwa umma kwamba serikal ina nia ya dhati ya kumaliza rushwa bila kujali mpasuko wa kiitikadi uliopo."
Mwanaharakati wa haki za binadamu Patson Dzamara alisema kuwa kukamatwa hakuwa na uhusiano na rushwa lakini ni muendelezo wa vita vya mpasuko ndani ya chama tawala cha Zanu PF.
"Hakuna namna yoyote kuwa hii kamata kamata inaweza kuwa juu ya rushwa," alisema.
"Hauhitaji akili nyingi kutambua kwamba Zanu PF ni pango la rushwa, lakini unapomwona mtu mmoja mharifu akimkamata mwingine basi lazima ujue sio kuhusu rushwa."
"...Kwao wanataka tuamini kwamba ni wale tu waliokuwa katika G40 ni wala rushwa ni utani usiochekesha wa kitoto. "
Mnangagwa ameahidi kuondokana na rushwa, akisema kuwa ni moja ya sababu za uchumi wa Zimbabwe kuwa 'bomu'
CHANZO:
Comments
Post a Comment