Maduka makubwa ya 'Halal' nchini Ufaransa yamefungwa kwa sababu ya kukataa kuuza pombe na nyama ya nguruwe.
Maduka hayo yanayosifika kwa kuwa na bei nafuu za bidhaa huko Colombes, Paris yalitishiwa kufungwa mwaka jana kwa kukiuka sheria ya kupanga majengo ambayo inahitaji maduka ya aina hiyo kuuza bidhaa za aina zote.
Lakini mmiliki wake, Bwana Soulemane Yalcin alikataa kuuza pombe na nguruwe na mahakama sasa imeamua kuwa mkataba wake wa kupanga ufutwe.
Mahakama ya Nanterre iliamua Jumatatu kwamba alishindwa kufikia 'mahitaji ya wenyeji wote.'
Uamuzi ulikuja baada ya wananchi kulalamika kwamba hawataweza tena kupata bidhaa mbalimbali baada ya maduka makubwa ya Halal kuwepo kama maduka makubwa mbadala baada mengine ya kawaida yaliyokuwepo hapo awali.
Mwaka jana Nicole Goueta, meya wa Colombes, alitembelea duka ili amhimize Bwana Yalcin kuanza kuuza pombe na nguruwe.
Afisa mtendaji mkuu wa ofisi ya Meya, Bwana Jerome Besnard, alisema kuwa alimwomba mmiliki 'kuchanganya' bidhaa zake za kuuza baada ya malalamiko kutoka kwa wenyeji.
Aliongeza kuwa eneo hilo linataka 'mchanganyiko wa jamii' ambapo kila mtu anaweza kupata chaguo la bidhaa.
Wakazi wengi wakongwe hawawezi kukamilisha mahitaji yao yote kwenye duka hilo jipya, kufuatia kufungwa kwa maduka makubwa ya zamani.
Hii imewafanya waweze kusafiri kwenda mbali kwenye maduka mengine kununua nguruwe na pombe.
Akizungumza na Le Parisien, Bwana Yalcin, ambaye alifungua duka lake mwezi Aprili 2015, alitetea uamuzi wake wa kuuza bidhaa hizo.
Alidai kwamba alikuwa tu akihudumia mahitaji ya wateja wake katika eneo hilo.
Alisema:
"Ninatazama karibu na mimi na ninatafuta kile ninachokiona.Sheria Kupanga majengo inataka 'kuuza vyakula vya aina zote na shughuli zinazohusiana' - lakini yote inategemea jinsi unavyoitafsiri 'shughuli zinazohusiana'."
Bwana Yalcin aliongeza kuwa maduka mengine ya kuuza pombe katika eneo hilo yanakabiliwa na 'matatizo ya usalama' na kudai takwimu za mauzo ya Franprix ilionyesha kuna 'hasara katika idara ya chakula'.
Mmiliki huyo ameamriwa kulipa ada ya mahakama ya euro 4,000, na kuama kwenye majengo.
CHANZO:
dailymail.co.uk
Comments
Post a Comment