Mwana wa rais wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi, Saif Al-Islam Gaddafi, anajitayarisha kurudi kwenye siasa katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini, ripoti zimesema.
Saif al-Islam Gaddafi alitolewa jela mwezi Juni baada ya kushikiliwa kwa miaka sita na wanamgambo wa mji wa Zintan kufuatia uasi wa wanamgambo waliokuwa wakisaidiwa na majeshi ya Nato nchini Libya mwaka 2011.
Mwanasheria wa Saif al-Islam Khaled al-Zaidi, akizungumza katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis, aliwaambia waandishi wa habari Saif al-Islam anarudi kwenye medani za kisiasa kwenye nchini Libya, akiongeza kuwa alikuwa na afya njema.
"Anafanya kazi za siasa kutoka kwenye ngome yake Libya, na makabila, pamoja na miji, na wabunge," Zaidi alisema.
"Ana afya nzuri ... katika hali ya juu. Hali yake ya matibabu na kisaikolojia ni nzuri.
"Lengo ni kufikia amani Libya," alisema Zaidi.
"Anafuatilia mambo ya Libya karibu kila siku."
Bwana Gaddafi, ambaye alisoma katika Shule ya Uchumi ya London, anajulikana kama 'mtu wa kisasa', lilisema gazeti la Uingereza 'The Guardian'.
Saif al-Islam anashutumiwa kuwaua waandamanaji wakati wa mapinduzi ya Libya ya mwaka 2011, ambayo yalimtoa madarakani na kumwua baba yake, Muammar Gaddafi.
Mahali halisi alipo sasa Saif al-Islam bado hapajulikani.
CHANZO:
wikileaksnews.co
Comments
Post a Comment