Joto limezidi kupanda katika uhusiano wa mke wa rais wa zamani wa Zimbabwe, Bibi Grace Mugabe na mme wake baada ya ndugu wa mzee Mugabe kudai kuwa shemeji yao amekua akidhohofisha uhusiano kati ya ndugu kwa kusababisha migogoro isiyoisha baina yao.
Baadhi ya ndugu hao wa mzee Robert Mugabe wameripotiwa kuwa walivunja mahusiano na shemeji yao Grace Mugabe zaidi ya miaka miwili iliyopita.
Kwa mujibu wa tovuti ya "Sauti ya Amerika" (VOA), jamaa za Mugabe wamemshutumu Grace kwa "kutokuheshimu wazee wa familia, pamoja na kuonyesha na kupanda mbegu za ugomvi ndani ya familia".
Mjomba wa Mugabe Ben Matibiri alidai kwamba Grace alimpuuza kila mtu katika familia ya Mugabe "akijaribu kukwapua madaraka wakati wote". Hii, alisema kuwa ni kinyume chake cha mke wa kwanza wa Mugabe, marehemu Sally Hefron Mugabe, ambaye alimuelezea kama "binti kubwa" kwa familia.
Hii ilikuja kama taarifa juu ya habari za mwishoni mwa wiki zilizodai kwamba Grace alikuwa akilalamika kuhusu jinsi familia yake, biashara na washirika walivyokuwa wakitendewa baada ya kuanguka kwa utawala wa mumewe.
Kwa mujibu wa gazeti la "The Zimbabwe Independent", ingawa familia ya Mugabe ilionekana kuwa na ukimya na utulivu mbele ya umma, Grae Mugabe alikuwa analalamika chini chini kuhusu jinsi familia yake na familia za washirika wake wanavyotendewa.
Grace alikuwa akilalamika kwa Rais Emmerson Mnangagwa na Kamanda wa Ulinzi wa Zimbabwe Constantino Chiwenga kupitia wapatanishi, kiongozi wa Katoliki Baba Fidelis Mukonori na Gavana wa zamani wa Benki ya Zimbabwe Gideon Gono.
Grace alilalamika juu ya vitisho kwa biashara na mali yake, akirejea kwenye makubaliano yaliyofikiwa kwa siri kama sehemu ya mpango wa Mugabe kujiuzulu.
CHANZO:
Comments
Post a Comment