Burundi inakusudia kuongeza fedha kwa ajili ya uchaguzi mwaka 2020 kwa kupunguza sehemu ya mishahara ya watumishi wa umma na kuchukua michango moja kwa moja kutoka kwa wananchi, waziri wa serikali alisema Jumatatu.
Mpaka mwaka 2015, Burundi ilikuwa inatumia misaada kutoka nje ya nchi kulipia gharama za uchaguzi, lakini wafadhili wamesimamisha misaada yao tangu mgogoro wa kisiasa ulipotokea wakati Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza na kugombania urais kwa muhula wa tatu.
Pascal Barandagiye, waziri wa mambo ya ndani, alisema serikali pia itakuwa ikitafuta michango kutoka kwa kila kaya, ambayo italipa hadi faranga 2000 (US $ 1.14) kwa mwaka.
Wastani wa mapato ya kila mtu kitaifa yalikuwa dola za Marekani 280 kwa mwaka 2016, na karibu asilimia 65 ya idadi ya watu wanaishi chini ya mstari wa umasikini, kulingana na takwimu za Benki ya Dunia.
"Jumla ya gharama za uchaguzi bado haijulikani ...
"Mchango huo unapaswa kupewa kwa hiari, haipaswi kuonekana kama kodi ya kichwa."
Wanafunzi wenye umri wa kupiga kura watachangia faranga 1000 sawa na dola za kimarekani 0.57($0.57) kila mwaka.
"Watumishi wa umma watachangia angalau asilimia kumi ya mishahara yao ya kila mwezi,"
Barandagiye alisema.
"Misaada ya kigeni pia inakubaliwa",alisema.
Burundi imekuwa imesababishwa na mgogoro wa kisiasa tangu Aprili 2015, wakati Rais Nkurunziza alitangaza kuwa atagombea urais kwa muhula wa tatu, ambayo upinzani huo umelisema ni ukiukaji wa sheria na pia mpango wa amani wa 2005 uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka 12.
Alishinda kwa kiasi kikubwa katika uchaguzi huo uliosusiwa na wapinzani, lakini maandamano yalisababisha machafuko na uharibifu wa miundombinu ya serikali na raia.
Zaidi ya watu 700 wameuawa na 400,000 wamekimbilia katika nchi za jirani.
Uchumi umeshuka.
Taifa linalotegemea misaada sasa linategemea ukusanyaji wa kodi ya ndani na mapato ya kawaida kutokana na mauzo ya kahawa na mauzo ya chai.
Wahisani muhimu, kama Umoja wa Ulaya, wamekata mkono misaada ya kifedha moja kwa moja kwa serikali kutokana na mashtaka ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu na kuvunjwa kwa upinzani, ambao Burundi inakataa.
Mwishoni mwa mwezi wa Oktoba, baraza la mawaziri la Burundi lilipitisha rasimu ya sheria inayotaka kubadilisha katiba ya sasa kuruhusu Nkurunziza kugombea urais kwa muhula wa nne katika uchaguzi wa 2020.
Marekebisho yaliyopendekezwa, ambayo yanaweza kwenda kwenye kura ya maoni kwa mwaka ujao, yanajaribu kufuta kikomo cha mihula miwili na kuongeza muda wa urais kuwa miaka saba.
CHANZO:
Comments
Post a Comment