Hadithi za mashambulizi ya usiku wa manane na 'Wanyonya damu' (Vampires) za kunyonya damu zinaendelea kusababisha matatizo nchini Malawi, kusini mashariki mwa Afrika.
Madai 'ya waathirika' wanashambuliwa usiku na 'wanyonya damu' yamesababisha vurugu za wananchi kuchukua sheria mkononi na vifo katika sehemu za kusini za nchi hiyo.
Watu takribani saba wameuawa katika wilaya moja, na mapema mwaka huu, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wa kujitolea kutoka Marekani waliondolewa katika eneo hilo.
Wakati wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliporudi sasa, hadithi za mashambulizi ya kunyonya damu zinaendelea.
Jamiya Bauleni, mama mwenye umri wa miaka 40, alisema kuwa mshambulizi aliingia nyumbani kwake na kunyonya damu yake nyumbani kwake katika wilaya ya Thyolo.
'Hii sio kusikia,' aliuambia umati wa watu katika kijiji cha Ngolongoliwa kusini mwa nchi hiyo ambayo imekuwa katika hali ya hofu hivi karibuni juu ya uvumi wa shughuli za 'wanyonya damu'.
"Najua damu yangu ilinyonywa. Niliona mwanga kwenye kona ya paa langu. Nilishindwa kusimama kutoka kitandani kwangu na nikasikia kitu cha kimetoboa mkono wangu wa kushoto, "alisema, akionesha karibu na kifua chake.
Hadithi yake ni sehemu ya mlolongo mrefu wa ushuhuda sawa nchini Malawi, ambapo imani katika uchawi na shughuli za vampire zinaenea na kusababisha watu kulipa kisasi kwa kujichukulia sheria mkononi na kuwaua watuhumiwa wa uchawi.
Bauleni, ambaye hufanya uuzaji wa chakula cha mchana, alisema kuwa kabla ya kuanguka na kupoteza fahamu alisikia mtu anayekimbia eneo hilo.
Alipelekwa kwenye kliniki na baadaye aliachiliwa baada ya kupewa virutubisho vya vitamini, lakini aliamua kutokuripoti shambulio hilo.
Uvumi wa kuwepo kwa 'wanyonya damu' unasemekana kutokea nchi jirani ya Msumbiji na kuvuka mpaka kuenea mpaka kwenye wilaya za Malawi za Mulanje na Phalombe, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa.
Watu takribani saba wameuawa katika wilaya ya Mulanje baada ya kuwindwa, polisi wanasema.
Muathirika mmoja, Florence Kalunga, mwenye umri wa miaka 27, anasema alikuwa amelala pamoja na mumewe nyumbani kwake alipoona mwanga kama moto.
"Nilisikia mlango unafunguliwa... Nilihisi kitu kama sindano katika kidole changu, "alisema.
Watu wanaolengwa katika vurugu kulipa kisasi mara nyingi ni watu wenye utajiri katika sehemu za vijijini za nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ambapo umasikini umezoeleka na kiwango cha elimu ni duni sana.
Mjasiriamali Orlendo Chaponda alifanikiwa kukimbia mashambulizi wakati wanakijiji 2,000, baadhi yao waliokuwa wamebeba mapanga na mawe walipovamia nyumba yake huko Thyolo mnamo Septemba 30.
"Wao walisema nilikuwa nikiwahifadhi wanyonya damu,",
alisema Chaponda, ambaye alikuwa nje wakati huo.
"Wangeweza kuniua ikiwa wangenipata."
Aliwaita polisi ambao walitumia mabomu ya machozi ili kutawanya umati uliokua umezunguka nyumba yake kwa masaa matano.
"Hakuna ukweli juu ya wanyonya damu, ila watu wenye wivu na majambazi wanataka kuchukua nafasi hiyo kushambulia matajiri,"
Chaponda alisema.
"Ikiwa una gari nzuri, wewe ni mnyonya damu."
Shirika la huduma ya damu ya kitaifa ya Malawi - taasisi pekee iliyoruhusiwa na serikali kukusanya damu kwa ajiri ya hospitali kutoka kwa watu wanaojitolea - limesema kwamba uvumi wa matukio ya 'wanyonya damu' pia umeanza kurudisha nyuma shughuli za taasisi hiyo.
"Suala hili limeleta athari sana...limtuzuia kwenda kukusanya damu katika maeneo yaliyoathirika, "alisema Bridon M'baya, mkurugenzi wa huduma za matibabu.
Watu takribani 250 wamekamatwa nchini Malawi juu ya unyanyasaji wa watu, na wengine 40 walikamatwa juu ya makosa sawa na hayo katika nchi jirani ya Msumbiji.
Rais wa Malawi Peter Mutharika alilazimika kukubali kuwa kumekuwepo na tatizo hilo na kusisitiza kwamba serikali tayari imelidhibiti.
"Hakuna ushahidi wa wanyonya damu. Ni uwongo wenye nia ya kudhoofisha kanda, "alisema hivi karibuni.
"Wale wanaoeneza uvumi huu watapambana na sheria."
Anthony Mtuta, mwalimu msaidizi wa anthropolojia katika Chuo Kikuu cha Katoliki cha Malawi, alisema mizizi ya vitisho vya 'Wanyonya damu' imeanzia katika shida za uchumi na madara katika jamii'
"Ni matajiri dhidi ya masikini. Maskini wanaamini kuwa tajiri ni wenye tamaa na wananyonya damu za watu masikini,", alisema.
Malawi kwa kiasi kikubwa inategemea misaada ya kigeni, lakini baadhi ya wenyeji wanapokea misaada kwa mashaka.
"Kwa wanakijiji, hufikiri kwamba hakuna zawadi utaipata bure ... utailipa kupitia damu," alisema Mtuta.
McDonald Kolokombe, karani katika hifadhi ya misitu ya Likhubula ya serikali, alibainisha kuwa idadi ya watalii waliotembelea eneo la Mulanje imeshuka tangu katikati ya Septemba.
"Jamii hutegemea wageni kulisha familia zao kwa kufanya kazi kama kuongoza watalii na kuwauzia bidhaa", alisema.
"Tuna njaa kwa sababu ya uvumi mbaya juu ya 'wanyonya damu,' ", aliongeza muongoza watalii(tour guide), Eric John.
"Ni uongo mkubwa."
CHANZO:
hinnews.com
Comments
Post a Comment