Wananchi nchini Saudi Arabia kuanzia mwaka 2018 wataruhusiwa kwenda kwenye majumba ya sinema kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya miaka 30 ya kupigwa marufuku.
Wizara ya utamaduni na habari ya Saudi Arabia imesema itaanza kutoa leseni za filamu kutoka sasa na kwamba sinema za kwanza zitaanza kuoneshwa kuanzia Machi 2018.
"Hii inaashiria muda wa mabadiliko katika maendeleo ya uchumi wa kitamaduni katika Ufalme,"
Waziri wa Utamaduni na Habari Awwad Alawwad alisema katika taarifa hiyo.
"Ufunguzi wa sinema utafanya kazi kama kichocheo kwa ukuaji wa uchumi na uwiano; kwa kuendeleza sekta kubwa ya kitamaduni tutaunda fursa mpya za ajira na mafunzo, pamoja na kuimarisha chaguzi za burudani za Ufalme. "
Majumba ya sinema yalifungwa kwa mara ya kwanza katika miaka ya 1980, baada ya viongozi wa dini wengi wa kihafidhina walipodai kwamba sinema kutoka Magharibi na sehemu zingine zimejaa dhambi.
Mpaka mwaka 2030 Saudi Arabia itakuwa na majumba ya sinema zaidi ya 300 na skrini karibu 2,000, serikali ya Saudi imethibitisha.
Kuondoa marufuku ya leseni ya filamu ni juhudi za hivi karibuni za mpango wa mageuzi ya kijamii ya ufalme wa huo wa Kiislamu kama pia ikijaribu kuboresha muonekano yake duniani kote.
Miezi miwili tu iliyopita mwana wa mfalme aliyevikwa taji Mohammed bin Salman aliondoa sheria ya marufuku kwa wanawake wa Saudi kuendesha gari.
CHANZO:
wikileaksnews.com
Comments
Post a Comment