Kiongozi wa upinzani wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika Kusini, afisa mkuu wa chama chake cha MDC amesema. Bw Tsvangirai, mwenye umri wa miaka 65, aliyekuwa waziri mkuu, alilipotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na saratani ya koloni. "Amefariki jioni hii, familia yake imenitaarifu" Makamu wa Rais wa MDC, Elias Mudzuri aliliambia shirika la habari la Uingereza, Reuters. Morgan Tsvangirai alizaliwa mnamo Machi 10, 1952 huko Gutu, Zimbabwe. Baba yake alikuwa mfanyakazi wa mgodi, fundi, na mkulima. Alihudhuria Shule ya Msingi ya Guco ya St. Marks. Kisha alihamishiwa Shule ya Msingi ya Chikara Gutu. Kwa elimu yake ya sekondari, alihudhuria Shule ya High Gokomere. Alikuwa waziri mkuu katika serikali ya mseto ya Zimbabwe tangu 2009 hadi 2013. Katika kazi yake ya awali alionekana kuwa mfanyakazi mwenye bidii sana na alifanya kazi katika mgodi wa madini ya nickel( kwa zaidi ya muongo mmoja. Alipanda cheo haraka kutambuliwa na akain