Skip to main content

Posts

KIONGOZI MKUU WA UPINZANI NCHINI ZIMBABWE, MORGAN TSVANGIRAI AMEFARIKI DUNIA.

Kiongozi wa upinzani wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika Kusini, afisa mkuu wa chama chake cha MDC amesema. Bw Tsvangirai, mwenye umri wa miaka 65, aliyekuwa waziri mkuu, alilipotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na saratani ya koloni. "Amefariki jioni hii, familia yake imenitaarifu"  Makamu wa Rais wa MDC, Elias Mudzuri aliliambia shirika la habari la Uingereza, Reuters. Morgan Tsvangirai alizaliwa mnamo Machi 10, 1952 huko Gutu, Zimbabwe. Baba yake alikuwa mfanyakazi wa mgodi, fundi, na mkulima. Alihudhuria Shule ya Msingi ya Guco ya St. Marks. Kisha alihamishiwa Shule ya Msingi ya Chikara Gutu. Kwa elimu yake ya sekondari, alihudhuria Shule ya High Gokomere. Alikuwa waziri mkuu katika serikali ya mseto ya Zimbabwe tangu 2009 hadi 2013. Katika kazi yake ya awali alionekana kuwa mfanyakazi mwenye bidii sana na alifanya kazi katika mgodi wa madini ya nickel( kwa zaidi ya muongo mmoja. Alipanda cheo haraka kutambuliwa na akain
Recent posts

BAYERN MUNICH WANAJENGA VYUMBA VYA HOTELI NDANI YA UWANJA.

Huu ndio utakaokuwa muonekano wa vyumba hivyo kwa ndani. Picha: Mariot International. Kama sehemu ya mpango wa miaka mingi ya Bayern na  kampuni kubwa ya hoteli za Mariot na Courtyard, mashabiki hivi karibuni wataweza kupata fursa ya kukaa katika vyumba ambavyo vina dirisha linaloangalia uwanja wa Alianz Arena moja kwa moja. Vyumba hivyo vya kifahari vya kulala vitakuwa na kitanda cha kikubwa na seti ya televisheni - tu ikiwa umechoka na hat-trick za Robert Lewandowski. Pia kutakuwa na mahali pa moto ambayo ni maalumu kwa siku za mechi kwenye majira ya baridi. Mkurugenzi Mtendaji wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge alisema: "Tunafurahia bidhaa mbili zinazoongoza kama hoteli Courtyard zinazomilikiwa na kampuni ya Marriott na FC Bayern kuingia katika ushirikiano huu wa muda mrefu kibiashara. "Tunapendezwa na bidhaa mbili zinazoongoza kama Courtyard na Marriott na FC Bayern kuingia katika ushirikiano wa muda mrefu," "Kutokana na kwamba Marri

MADAI YA CUBA KWAMBA WAZIRI MKUU WA CANADA NI MTOTO WA FIDEL CASTRO.

Pichani ni waziri mkuu wa Canada, Justin Trudeau (kushoto), na Rais wa zamani wa Cuba, Hayati Fidel Castro (kulia). Maelezo yaliyoandikwa na mtoto wa kwanza wa rais wa zamani wa Cuba , Fidel Castro, kabla ya kujiua yamelishtua taifa la Cuba wiki hii. Maelezo hayo yaliyoandikwa na mtoto huyo mkubwa wa mwanamapinduzi na rais wa zamani wa nchi hiyo yalikuwa ya kushangaza baada ya  kuwa na madai ya kuwa Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau ni mtoto wa nje wa baba yake marehemu Fidel Castro. Maelezo hayo yaliyoandikwa kwa mkono na mtoto huyo wa Fidel Castro aliyejiua siku chache zilizopita kwa msongo wa mawazo, Fidel Castro Diaz-Balart, aliyekuwa na umri wa miaka 68, yalionekana kuthibitisha uvumi wa muda mrefu nchini Cuba kwamba Fidel Castro ni baba wa damu wa waziri mkuu wa sasa wa Canada, Justin Trudeau ikiwa ni matokeo ya uhusiano wa siri wa kimapenzi na mke wa mwanasiasa maarufu wa Canada, Pierre Trudeau, Margaret Trudeau mwaka 1970. Kifo cha mwanasayansi wa nyuk

SABABU YA SOKO LA NYAMA YA MBWA KUONGEZEKA NCHINI CHINA.

Kila mwaka wakati wa msimu wa majira ya joto, tamasha la kula mbwa linafanyika Yulin, jiji lililo katika jimbo la kusini mwa China la Guangxi.  Tukio la mwaka jana lilimalizika na utata usio wa kawaida. Picha za mbwa wakichinjwa kikatili na kukaangwa zilisababisha gumzo kubwa ulimwenguni kote. Tamasha la Nyama ya Mbwa la Jinhua Hutou, kama linavyoitwa, lilifungwa ghafla wiki chache zilizopita. Wanaharakati wa haki za wanyama na wabunge wa Marekani walitaka Uchina kupiga marufuku kula na mbwa na paka, kama vile Taiwan alivyofanya mwaka 2017.  Serikali za mitaa za Yulin zilichukua hatua za kuzuia na kuficha baadhi ya shughuli za baadhi ya shughuli hizo kama vile kuuza mbwa katika masoko ya chakula.  Hata hivyo, tamasha hilo lilifanyika na kufana zaidi ya miaka mingine.  Kwa nini tabia hii isiyo ya kawaida kwa nchi nyingine imekuwa maarufu sana nchini China? Nyama ya mbwa haijawahi kuwa kitu cha kawaida katika chakula cha Kichina. Tofauti na sehemu nying

TRUMP NA KIM JONG-UN FEKI WAHUBIRI AMANI KATIKA SHEREHE ZA UZINDUZI WA OLIMPIKI.

Waigaji wa Rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un walikua wakihubiri amani katika sherehe za uzinduzi wa michezo ya Olympiki kwa majira ya baridi(Winter Olympic) jijini Pyeong Chang, Korea ya Kaskazini kabla ya kutolewa nje na wanausalama. Watu hao walionekana kwa muda mfupi katika jukwaa la uwanja huo mkuu wa Pyeongchang, Korea Kusini ili kuwasalimu watu. Waigaji hao ambao wote walikataa kutoa majina yao halisi - walikuja kwenye sherehe ya ufunguzi -   "kuonyesha dunia, hii ndio amani inaweza kuonekana kama viongozi hao wawili watakapokutana,"  alisema Kim bandia. Trump bandia alimwiga Rais Trump kwa kuvaa kofia nyekundu ya mpira wa magongo (baseball), lakini ikiwa imeandikwa "USA" sio "Make America Great again"(Unda Amerika Kuu tena) kauli mbiu ambayo mara nyingi huandikwa kwenye mavazi na matangazo ya Trump. Pia alivaa tai ndefu ya rangi nyekundu kama ambavyo rais Trump mwenyewe hupendele

MWANAMUZIKI MAARUFU WA UGANDA, "RADIO", AMEFARIKI DUNIA.

Mwanamuziki wa Uganda Moses Ssekibogo, anajulikana kama Mowzey Radio wa kundi la Goodlyfe Crew amefariki. Promota Balaam Barugahara alimwambia mwandishi wa gazeti la Monitor kwamba Radio alikufa Alhamisi saa 12 alfajili. Redio amefariki kwenye Hospitali ya Uchunguzi huko Kampala ambako alikuwa amelazwa baada ya kudaiwa kupigwa mpaka kupoteza fahamu baada ya kupigana huko De Bar, ukumbi maarufu wa starehe mjini Entebbe wiki iliyopita. Redio alipata majeraha baada ya kupigana bar na mmoja wa mabaunsa(walinzi) ambao walimpiga hadi kufikia kiwango cha kuanguka na kuvunja shingo yake. Kisha alikimbizwa kwenda Hospitali ya Nsambya ambako madaktari walikataa kumpokea kwa sababu alitaji kupelekwa kwenye hospitali ye huduma za ICU. Marafiki zake wakampeleka kwenye Kliniki ya Uchunguzi kwenye barabara ya Buganda, Kampala ambako alikuwa akipata matibabu. Radio alipokuwa amelazwa akiwa hana fahamu. Radio (aliyezaliwa kama Moses Nakintije Ssekibogo) mnamo 1 Januari

RAPA SNOOP DOGG AMETHIBITISHA MIPANGO YA KUHAMIA UGANDA.

Msanii wa muziki wa Hip Hop wa Marekani, Calvin Cordozar Broadus.Jr. maarufu kama Snoop Dogg amethibitisha kuwa anataka kuhamia Uganda baada ya rais wa Marekani, Donald Trump kudaiwa kuziita nchi za Afrika 'Shimo la Choo' . Snoop Doggy Dogg pia ni mwimbaji, mwandishi wa nyimbo, mtayarishaji wa muziki, mtangazaji katika televisheni, na mwigizaji wa filamu ambaye alianza kupata umaarufu mkubwa katika muziki mwaka 1992 wakati alipogunduliwa na mtayarishaji Dr.Dre, na kushiriki katika nyimbo za Dr.Dre kama "Deep Cover", na kisha kwenye albamu ya kwanza ya Dr.Dre, ' The Chronic' . Kwa sasa tayari ameshauza albamu zaidi ya milioni 23 nchini Marekani na albamu milioni 35 duniani kote. Mmarekani huyo mweusi mwenye miaka 46 wa ambaye anajulikana kwa nyimbo zake za maarufu kama; The next episode, Drop it like it’s hot, beautiful, Lay low,  nk Juzi alirekodi kipande cha video na kukisambaza akisema kuwa anataka kuhamia chini Uganda. Tazama V