JOHN PAUL MWIRIGI . Kijana mwenye umri wa miaka 23, John Paul Mwirigi, ana nafasi kubwa ya kuwa kijana mdogo kabisa kua Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Kenya iwapo atatangazwa kushinda kiti cha ubunge wa Igembe Kusini katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8. Mwirigi, amabae ni mgombea wa kujitegemea, anaongoza kwa kura zaidi ya 3,000 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Joseph Miriti Rufus Mwereria, ambaye ni mgombea kwa tiketi ya Chama cha Jubelee. Mpaka kufikia saa 7:50 jioni Jumatano, Mwirigi alikuwa na kura 19,366, ikilinganishwa na mpinzani wake wa kisiasa, Mwereria, ambaye - wakati huo huo - alikuwa na kura 15,977, ambayo ni asilimia 95.14 ya matokeo kutoka vituo vya kupigia kura. Mkutano wa kampeni ya Mwirigi ulikuwa na hisia ya unyenyekevu, aliweza kuzunguka kwa miguu mlango kwa mlango, kuwakumbusha wapiga kura kuwatambulisha wapiga kura kumtambua kwa sweta lake la kijivu lenye mstari mweusi kifuani katika karatasi za kura. Mwirigi kamwe hakuchapis...