IGP ERNEST MANGU. |
Ikiwa ni siku moja tu tangu Kurugenzi ya Habari Ikulu ilipotoa taarifa ya kumpandisha cheo mkuu wa polisi wa kanda maalumu ya Dar es Salaam, kamanda Simon Sirro kuwa mkuu wa polisi Tanzania na kutoa tamko kwamba mkuu wa jeshi hilo wa sasa Inspekta Jenerali Ernest Mangu atapangiwa kazi nyingine, Taarifa hiyo imepokelewa kwa mawazo tofauti tofauti na wananchi hasa ikiwa wengi wanajiuliza ni kwanini IGP Mangu ametolewa katika nyadhifa hiyo ya juu kabisa kwenye jeshi la polisi kabla ya muda wake wa kustaafu kufika !!!.
BARUA KUTOKA IKULU KWA WAANDISHI WA HABARI. |
Chanzo cha blog yetu (Kioo17) siku ile ile ya jana 28 Mei 2017 ,kilibahatika kupata maoni ya mchambuzi nguli wa mambo ya siasa Bwana Malisa GJ alitukumbusha kwamba kuna mwanahabari wa gazeti la "MwanaHalisi" bwana Charles William Alibashili haya ya jana takribani miaka miwili iliyopita !!!.
SOMA HII;
MALISA GJ:
Mdogo wangu Charles William aliandika miaka miwili iliyopita kuwa Ernest Mangu atang'olewa ktk nafasi yake ya IGP na kupewa Simon Siro. Soma makala hii iliyoandikwa na Charless William na kuchapwa na gazeti la Mwanahalisi la December 21, mwaka 2015.
_____________________________________________
JGP MANGU KUNG'OKA
Na Charles William,
MwanaHALISI - Desemba 21, 2015.
__________________________________
Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dk. John Magufuli anajiandaa kufanya mabadiliko makubwa ndani ya Jeshi la Polisi kwa kumuondoa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu.
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa mmoja wa maofisa wa Ikulu zinaeleza kuwa Dk. Magufuli sasa anahitaji kuwa na mkuu mpya wa Jeshi hilo huku IGP Mangu akitarajiwa kupewa ubalozi katika mojawapo ya nchi za Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara na Naibu wake Abdurahmani Kaniki akitarajiwa kushushwa ngazi na kuwa mkuu wa polisi katika mkoa mojawapo kanda ya ziwa.
Iwapo Rais Magufuli atabadilisha mkuu wa jeshi hilo, IGP Mangu atakuwa amelitumikia jeshi hilo kwa muda wa miaka miwili tu baada ya kuteuliwa na Rais Kikwete kushika wadhifa huo Desemba 30, 2013 akitokea ofisi ya Polisi wa kimataifa (Interpol) jijini Nairobi, Kenya.
Wanaotajwa kuwa kwenye nafasi ya kumrithi IGP Mangu ni pamoja na mkuu wa Operesheni wa polisi, Simon Siro na mkuu wa Interpol Gustav Babile.
Kwasasa waliopo katika nafasi za juu za jeshi hilo ni kamishna Glodwig Mtweve (fedha na utawala), Mussa Ally Mussa (Polisi Jamii makao makuu), Thobias Andengenye (utawala na utumishi) na Diwani Athumani (Mkuu wa intelijensia ya jinai DCI).
Haya yanakuja ikiwa ni wiki mbili tu tangu Rais Magufuli afanye mabadiliko ya kushitua akimuhamisha Kamishina wa Operesheni na Mafunzo Paul Chagonja na kumpeleka kuwa mkuu wa jeshi la zimamoto na uokoaji huku mkuu wa idara ya intelijensia Valentino Mlowola akiteuliwa kuwa kaimu mkurugenzi wa TAKUKURU.........
______________
©Charles William.
Comments
Post a Comment