DR.SERGIO CANAVERO. |
Dr.Sergio Canavero ,Daktari bingwa wa upasuaji (Neurosurgeon) kutoka Italia, ametangaza kufanya operesheni ya kwanza ya kupandikiza kichwa cha binadamu kutoka mwili mmoja kwenda mwingine.
Akizungumza na gazeti la OOOM la Ujerumani, Dr.Canavero amesema operesheni hiyo itafanyika mwezi Desemba mwaka huu nchini China na jopo la madaktari 80 kwa masaa 36 na itagharimu dola milioni 10 (takribani shilingi bilioni 21 za kitanzania).
Tayari mtu wa kujitolea kufanyiwa operesheni hiyo amepatikana.Mtu huyo anaitwa Valery Spiridonov.Spiridonov ni mzaliwa wa Urusi anaesumbuliwa na ugonjwa unaoitwa Werning-Hoffman,ugonjwa uliosababisha misuli na mishipa yake ya kuanzia shingoni mpaka miguuni kushindwa kufanya kazi kiusahihi.Spiridonov anaishi kwenye kiti cha wagonjwa(wheelchair) ,hawezi hata kula mwenyewe.
VALERY SPIRIDONOV. |
Dr Canavero ameelezea jinsi watakavyo hamisha kichwa cha Spirinov na kukipandikiza kwenye mwili wa mtu mwingine ambae ubongo wake umekufa.
Akifafanua jinsi watakavyo tekeleza operesheni hiyo, Dr.Canavero amesema kwanza watapooza joto la mwili wa Spiridonov mpaka kufikia Fahrenheit 50 ( nyuzi joto 10) ili na kutumia saa moja kukikata kichwa kwa nyembe maalum (Transparent Diamond Blades) na kukihamisha kabla ubongo haujafa.Pia amefafanua kwamba kichwa hicho kitaunganishwa na uti wa mgongo wa mwili mpya kwa kutumia kemikali iitwayo Polyethylene Glycol (PEG).
Dr.Canavero anaamini operesheni hiyo itafanikiwa kwa asilimia 90 baada kufanikisha kupandikiza kichwa cha panya mdogo kwenye mwili wa panya mkubwa miezi michache iliyopita.
Pia, anaami hivyo kutokana na kufanikiwa kwa operesheni ya kupandikiza kichwa kwa nyani iliyofanywa na Dr.Xiaoping Ren wa Harpin Medical University.
DR.CANAVERO AKIWA NA DR.XIAOPING REN ,ALIYEFANIKISHA KUPANDIKIZA KICHWA KWA NYANI. |
Hata hivyo jaribio hilo la Dr.Canavero limepokewa kwa maoni tofauti na watu mbalimbali akiwemo akiwemo mtaalamu Arthur Caplan wa New York University ambae taadharisha kwamba ni kitendo cha hatari na cha kipumbavu sababu kinahatarisha maisha ya mgonjwa.
CHANZO:Christian Gollayan,New York Post.
William McKinney, Edgylabs.com
Comments
Post a Comment