Skip to main content

AFANDE SELE "AMCHANA" MH.ABOOD.


AFANDE SELE.

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop kutoka Morogoro ,Selemani Msindi maarufu kama "Afande Sele" ,Juzi amejikuta akiingia kwenye mjadala mkali katika mitandao ya kijamii hususani Facebook baada ya kumkosoa Mbunge wake wa Morogoro mjini kuhusu usafi wa mji huo.
MBUNGE WA MOROGORO MJINI (CCM),MH.AZIZ ABOOD.

          Afande Sele ambae aligombania ubunge wa jimbo hilo la Morogoro mjini mwaka 2015 kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo ,alizua mjadala huo baada ya mji huo kushika nafasi ya 33 katika orodha ya miji michafu duniani kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

TA




Comments

Habari Nyingine Kutoka Kioo17 Swahili;

ORODHA YA NCHI ZA KWANZA NA ZA MWISHO KWA AMANI DUNIANI.

Marekani:  Ripoti ya Taasisi ya Uchumi na Amani imepata mataifa kumi tu ulimwenguni ambayo hayapo katika vita na migogoro kabisa. Kwa mujibu wa Ripoti ya Kimataifa ya Amani 2016, Botswana, Chile, Costa Rica, Japan, Mauritius, Panama, Qatar, Uswisi, Uruguay na Vietnam ndio nchi pekee ambazo hazipo kwenye vita wala migogoro yeyote ile ya kuhatarisha amani.. Iceland inaongoza orodha ya nchi zinazoongoza kwa amani ulimwenguni, ikifuatiwa na Denmark, Austria, New Zealand, Ureno, Jamhuri ya Czech, Uswisi, Canada, Japan na Slovenia - wakati Marekani ikiwa kwenye nafasi ya 103. Palestina imepanda kutoka nafasi ya 163 mpaka nafasi ya 148. Syria iliyoharibiwa na vita imewekwa chini ya orodha, chini kuliko Sudan Kusini, Iraq, Afghanistan, Somalia, Yemen, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ukraine, Sudan na Libya. "Ripoti inalinganisha amani duniani kwa kutumia mandhari tatu pana: hali ya utulivu na usalama katika jamii; kiwango cha mgogoro wa ndani au wa kimataifa; na kiwango cha kije...

TRUMP NA KIM JONG-UN FEKI WAHUBIRI AMANI KATIKA SHEREHE ZA UZINDUZI WA OLIMPIKI.

Waigaji wa Rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un walikua wakihubiri amani katika sherehe za uzinduzi wa michezo ya Olympiki kwa majira ya baridi(Winter Olympic) jijini Pyeong Chang, Korea ya Kaskazini kabla ya kutolewa nje na wanausalama. Watu hao walionekana kwa muda mfupi katika jukwaa la uwanja huo mkuu wa Pyeongchang, Korea Kusini ili kuwasalimu watu. Waigaji hao ambao wote walikataa kutoa majina yao halisi - walikuja kwenye sherehe ya ufunguzi -   "kuonyesha dunia, hii ndio amani inaweza kuonekana kama viongozi hao wawili watakapokutana,"  alisema Kim bandia. Trump bandia alimwiga Rais Trump kwa kuvaa kofia nyekundu ya mpira wa magongo (baseball), lakini ikiwa imeandikwa "USA" sio "Make America Great again"(Unda Amerika Kuu tena) kauli mbiu ambayo mara nyingi huandikwa kwenye mavazi na matangazo ya Trump. Pia alivaa tai ndefu ya rangi nyekundu kama ambavyo rais Trump mwenyewe hupendele...

STAR TV YAFUNGIWA NA TRA KWA KUKWEPA KODI.

Mamlaka ya mapato Tanzania inadaiwa kuifungia Radio Free Africa ya Mwanza inayomilikiwa na Antony Dialo kutokana na kudaiwa kodi kubwa. TRA wamewaondoa studio wafanyakazi wote na kuifunga radio hiyo. Kwa sasa ukiwasha radio utasikia matangazo ya kiingereza ya BBC. Diallo ni mwenyekiti wa CCM Mwanza na anadaiwa mamilioni ya kodi na TRA miaka mingi. Star Tv pia imekumbwa na sekeseke hilo. Ikumbukwe hii ndio TV pekee binafsi iliyokuwa ikipingana na MOAT na TEF katika sakata la RC Paul Makonda na walirusha kipindi maalum cha Makonda huku Jumuiya ya Wanahabari wakitangaza rasmi kujitenga na maswahibu yoyote yatakayokuja kuikuta RFA na Star TV. VYANZO : https://www.jamiiforums.com/threads/tra-waifungia-rfa-kwa-kudaiwa-kodi-ya-sh-bilioni-4-5.1283386/

MFALME WA GHANA ASABABISHA AFISA MKUU WA BENKI KUFUKUZWA KAZI.

Afisa mtendaji mkuu wa benki alifukuzwa kazi na kuchunguzwa na Shirika la Uhalifu wa Taifa baada ya kuweka pauni za Uingereza 350,000 ( £ 350,000 ) pesa taslimu aliyopewa na Mfalme wa Ghana. Mark Arthur wa benki ya Kimataifa ya Ghana Bigwig aliitwa kwenye nyumba ya Osei Tutu II huko Henley-on-Thames na kupewa £ 200,000 pamoja na $ 200,000 na kuagizwa aiweke kwenye akaunti ya benki ya Mfalme huyo. Licha ya noti hizo kuwa na namba za mfululizo zinazofuatana (consecutive serial numbers) Bwana Arthur alisema aliona kuwa haifai kumhoji mfalme na kwenda kuiweka benki kwa kutumia usafiri wa teksi ya uber. Punde baada ya Bwana Arthur kuweka pesa hiyo benki, taarifa ya utakatishaji wa fedha ilifika katika jiji la London, Uingereza na kugharimu ajira yake. Bwana Arthur alielezea kwenye taarifa yake ya ushahidi kuwa Mfalme alimwambia kwamba pesa hizo zimekusanywa kutoka kwenye akaunti za benki za nchini Ghana na kupelekwa Uingereza. Pia alidai kwamba Mfale alimpa $ 200,000 ili ...

KIONGOZI MKUU WA UPINZANI NCHINI ZIMBABWE, MORGAN TSVANGIRAI AMEFARIKI DUNIA.

Kiongozi wa upinzani wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika Kusini, afisa mkuu wa chama chake cha MDC amesema. Bw Tsvangirai, mwenye umri wa miaka 65, aliyekuwa waziri mkuu, alilipotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na saratani ya koloni. "Amefariki jioni hii, familia yake imenitaarifu"  Makamu wa Rais wa MDC, Elias Mudzuri aliliambia shirika la habari la Uingereza, Reuters. Morgan Tsvangirai alizaliwa mnamo Machi 10, 1952 huko Gutu, Zimbabwe. Baba yake alikuwa mfanyakazi wa mgodi, fundi, na mkulima. Alihudhuria Shule ya Msingi ya Guco ya St. Marks. Kisha alihamishiwa Shule ya Msingi ya Chikara Gutu. Kwa elimu yake ya sekondari, alihudhuria Shule ya High Gokomere. Alikuwa waziri mkuu katika serikali ya mseto ya Zimbabwe tangu 2009 hadi 2013. Katika kazi yake ya awali alionekana kuwa mfanyakazi mwenye bidii sana na alifanya kazi katika mgodi wa madini ya nickel( kwa zaidi ya muongo mmoja. Alipanda cheo haraka kutambuliwa na akain...

ORODHA YA NCHI 80 AMBAZO MTANZANIA ANARUHUSIWA KUINGIA BILA VIZA.

         Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza . Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza za kusafiria kama ilivyokuwa nchi za afrika Mashariki. Mhandisi Massauni amebainisha hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo kupitia tiketi ya CCM Rashid Shangazi aliyetaka kujua ni nchi ngapi ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza (viza on arrival). "Zipo nchi 16 kwa Afrika ambazo watanzania wanaweza kuzitembelea bila ya kuwa na viza na duniani zipo 67" alisema Masauni. Aidha Massauni amezitaja nchi hizo kuwa ni Benin, Burkina Faso, Cape Verde, Ivory Coast, Djibouti, Gabon, Gambia, Guinea, Guinea­Bissau, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Sierra Leone pamoja na Togo. Pamoja na hayo Masauni amesema...

KASHFA YA MAPENZI KATI MH.MBOWE NA WEMA SEPETU.

MH.FREEMAN MBOWE AKIWA NA WEMA SEPETU. Siku chache baada ya ile skendo ya ngono iliyosababisha wakili na mshauri wa Chama cha ACT -Wazalendo , Bwana Albert Msando kujiuzulu kwenye nyadhifa yake ya chama ,yameibuka mangine kwenye chama kikuu cha upinzani Tanzania ,CHADEMA ,baada ya kusambaa kwa kipande cha sauti kinachodaiwa kua ni mazungumzo kati ya mwenyekiti wa chama hicho na mbunge wa Hai Mh.Freeman Mbowe na Miss Tanzania 2006 ,mrembo Wema Isack Sepetu. SIKILIZA HIVI VIPANDE VYA SAUTI: Bonyeza hapa chini kusikiliza maongezi hayo yanayodaiwa kuwa ni kati ya Wema Sepetu na Mh.Freeman Mbowe; Bonyeza hapa chini kusikiliza majibu ya Wema Sepetu; Bonyeza hapa chini kusikiliza majibu ya Mh.Freeman Mbowe; VYANZO: Jamii Forums,                   YouTube.com,                   Perfect255.com.