Skip to main content

MWANAUME WA KWANZA KUPATA UJAUZITO NA KUJIFUNGUA !!!...


BWANA THOMAS BEATIE AKIWA MJAMZITO (2007).

Thomas Trace Beatie, ni mwanaume aliezaliwa tarehe 20 Januari,1974, kukulia na kuishi katika jiji la Honolulu, Hawaii ,Marekani.
      Mwaka 2007, Beatie ambae alikua mwanaume aliyemuoa mwanamke anaeitwa Nancy Gillespie aliishangaza dunia baada ya kupata ujauzito kwa kupandikizwa mbegu za kiume (artificial insemination).

      Ujauzito huo wa kushangaza wa Bw.Beatie uliwezekana baada ya hapo mnamo mwaka 2002 alipofanya operesheni ya kubadilisha jinsia (Gender Reassignment Surgery).

       Bwana Beatie mwenyewe alisema kwamba sababu ya kuamua kushika ujauzito na kuzaa mwenyewe ilikua ni baada ya kubainika kwamba mke wake (Nancy Gillespie) anamatatizo yanayomfanya ashindwe kupata ujauzito.
 
BWANA BEATIE BAADA YA KUJIFUNGUA MTOTO WA KWANZA ,MKEWE NANCY AKIWA AMEMSHIKA MTOTO.

  Ujauzito huo wa kwanza wa Bwana Beatie uliokua ni wa mapacha watatu ulitolewa na wataalamu kwa operesheni ya dharura baada ya kugundulika kwamba ulikua uko nje ya mfuko wa uzazi (Ectopic Pregnancy), hivyo alipoteza vichanga hivyo.
       Bwana Beatie bado hakukata tamaa!, Mwaka 2008 alijifungua mtoto wa kwanza ,Susan Juliette Beatie (wa kike) , Mwaka 2009 wa pili ,Austin Alexander Beatie (wa kiume) na mwaka 2010 alijifungua mtoto wake watatu na wa mwisho anaeitwa Jensen James Beatie (wa kiume).
   
BEATIE AKIWA NA MKE WAKE NANCY NA WATOTO WAO.

 Hata hivyo, Bwana Beatie aliachana na mke wake wa kwanza mwaka 2012 na mwaka 2016 alioa tena mke mwingine anaeitwa Amber Nicholas.
BWANA BEATIE AKIWA NA MKEWE MPYA AMBER NICHOLAS.


      Bwana Beatie wakati wa utoto aliwahi kushiriki mashindano ya urembo ya kike ya kumtafuta Miss Hawaii (Miss Hawaii Teen USA Pageant), aliwahi kupata umaarufu mkubwa katika michezo ya sarakasi (Aerobics) , kushiriki mashindano ya kutunisha misuli (Body building) na pia ni aliwahi kushiriki mashindano makubwa ya kupigana mpaka kupata mkanda mweusi (Black-belt) katika mchezo wa Taekwondo.
TAZAMA VIDEO YA MAPAMBANO YAKE HAPA:

      Bwana Beatie ambae ana shahada ya Sayansi ya afya (Pre-med) na shahada ya pili ya uongozi wa biashara (MBA) kutoka chuo kikuu cha Hawaii (Hawahii University) ni mmiliki wa kampuni ya mavazi na filamu ijulikanayo kama "Define Normal" na pia ni mwandishi na mwanaharakati wa kutetea haki za ndoa za jinsia moja (LGBT).
WATOTO WA BWANA BEATIE, KUANZIA KUSHOTO SUSAN, JENSEN NA AUSTIN. 

      Mwaka 2010 aliingizwa kwenye kitabu cha rekodi  cha Guinness (Guinness Book of records) kama mwanaume wa kwanza kupata ujauzito na kujifungua.

VYANZO: wikipedia.org

Comments

Habari Nyingine Kutoka Kioo17 Swahili;

ORODHA YA NCHI 80 AMBAZO MTANZANIA ANARUHUSIWA KUINGIA BILA VIZA.

         Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza . Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza za kusafiria kama ilivyokuwa nchi za afrika Mashariki. Mhandisi Massauni amebainisha hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo kupitia tiketi ya CCM Rashid Shangazi aliyetaka kujua ni nchi ngapi ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza (viza on arrival). "Zipo nchi 16 kwa Afrika ambazo watanzania wanaweza kuzitembelea bila ya kuwa na viza na duniani zipo 67" alisema Masauni. Aidha Massauni amezitaja nchi hizo kuwa ni Benin, Burkina Faso, Cape Verde, Ivory Coast, Djibouti, Gabon, Gambia, Guinea, Guinea­Bissau, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Sierra Leone pamoja na Togo. Pamoja na hayo Masauni amesema...

ORODHA YA NCHI ZA KWANZA NA ZA MWISHO KWA AMANI DUNIANI.

Marekani:  Ripoti ya Taasisi ya Uchumi na Amani imepata mataifa kumi tu ulimwenguni ambayo hayapo katika vita na migogoro kabisa. Kwa mujibu wa Ripoti ya Kimataifa ya Amani 2016, Botswana, Chile, Costa Rica, Japan, Mauritius, Panama, Qatar, Uswisi, Uruguay na Vietnam ndio nchi pekee ambazo hazipo kwenye vita wala migogoro yeyote ile ya kuhatarisha amani.. Iceland inaongoza orodha ya nchi zinazoongoza kwa amani ulimwenguni, ikifuatiwa na Denmark, Austria, New Zealand, Ureno, Jamhuri ya Czech, Uswisi, Canada, Japan na Slovenia - wakati Marekani ikiwa kwenye nafasi ya 103. Palestina imepanda kutoka nafasi ya 163 mpaka nafasi ya 148. Syria iliyoharibiwa na vita imewekwa chini ya orodha, chini kuliko Sudan Kusini, Iraq, Afghanistan, Somalia, Yemen, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ukraine, Sudan na Libya. "Ripoti inalinganisha amani duniani kwa kutumia mandhari tatu pana: hali ya utulivu na usalama katika jamii; kiwango cha mgogoro wa ndani au wa kimataifa; na kiwango cha kije...

WAZIRI GEORGE SIMBACHAWENE AJIUZULU.

Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene ametangaza kujiuzulu nafasi yake kutokana na kutajwa kwenye ripoti za uchunguzi wa tanzanite na almasi. Akiwasilisha ripoti yake kwa Waziri Mkuu Bungeni Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Bunge iliyoundwa kuchunguza biashara ya madini ya tanzanite, Dotto Biteko, alisema Simbachawene aulizwe ni kwa nini alitoa uhamisho wa hisa za Sky Associate bila kuhusisha wataalamu kwa sababu kamati ilishindwa kuelewa ni kwa nini alifanya hivyo. “Kwa muktadha huo, ridhaa iliyotolewa Januari 30, mwaka 2015 na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo, George Simbachawene, ina dosari za kisheria na ukiukwaji wa kiutendaji na utoaji wa ridhaa hii, unainyima Stamico kipaumbele cha kununua Kampuni ya TML. “Kwa msingi huo, kamati imebaini dosari zilizofanywa za kubadilisha watoa maamuzi wa Kampuni ya TLM, zilifanyiwa kazi katika ngazi ya Wizara ya Nishati na Madini chini ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Kamishna wa Nishati na Madini na idara za sher...

GRACE MUGABE : GABRIELLA ENGEL HUENDA ALIPIGWA SIKU KABLA.

MRS.GRACE MUGABE.  Picha na buzzsouthafrica.com JOHANNESBURG: Mke wa raisi wa Zimbabwe, Grace Mugabe, amekataa madai ya kumshambulia mwanamitindo wa Afrika Kusini Gabriella Engels na waya wa umeme katika chumba cha hoteli jijini Johannesburg mwezi uliopita, akisema kwamba msichana huyo alikua hajielewi na amelewa na alimshambulia kwa kisu. Taarifa hiyo ilisema Grace Mugabe, mwenye umri wa miaka 52, na mgombea kuchukua nafasi ya mume wake mwenye umri wa miaka 93 kama rais wa Zimbabwe, alikuwa anafikiri juu ya kufungua mashtaka ya jaribio la mauaji dhidi ya Engels. Kwa mujibu wa Engels, Mama Mugabe aliyekasirika aliingia ndani ya chumba ambako yeye na marafiki zake wawili walikua wakisubiri kukutana na Chatunga Mugabe tarehe 13 Agosti na kuanza kumshambulia kwa waya wa umeme. Picha zilizochukuliwa na mama yake baada ya tukio hilo zilionesha majeraha katika paji la uso na kichwa cha Engels. Pia alikuwa na michubuko katika mapaja yake. Katika madai yake, Mama Mugabe...

MCHEZAJI WA ZAMANI WA UINGEREZA AMESEMA ALICHEZA NA WACHEZAJI WATATU MASHOGA KWENYE TIMU.

Carl Hoefkens (jezi no.2) alichezea West Bromwich Albion na Stoke City wakati wa enzi zake ligi kuu ya England. Beki wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza amesema alicheza pamoja na wachezaji wenzake wawili wa mashoga ndani ya timu, na mmoja alikua na jina kubwa. Carl Hoefkens, West Bromwich Albion na Stoke City siku za nyuma, anasema wachezaji hao walikua wazi na hawakujificha kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ingawa bado hawajulikani kwasababu ya maombi yao wenyewe ya kuomba kutotangazwa. Justin Fashanu, ambaye alijiua mwaka 1998, alikuwa mchezaji wa mwisho wa kazi nchini England kuja nje kama mashoga - mwaka 1990. Hoefkens alipokua (kushoto), alipokua anachezea Stock  City. Hoefkens aliyecheza Uingereza kwa miaka minne, akiondoka mwaka 2009, alidai kuwa mchezaji mwenzake mmoja wa timu alikua anaweza kuja kwenye uwanja wa mafunzo ya klabu na mpenzi wake wa kiume  lakini aliwaomba wenzake kutokuwaambia watu wangine wa nje ya timu. 'Nilicheza pamoja n...

AMNESTY INTERNATIONAL YAIONYA SERIKARI YA TANZANIA.

Akizungumza kuhusu habari ya kwamba mkosoaji mkubwa wa serikari ya Tanzania ,Tundu Lissu kupigwa risasi kwenye makao makuu ya Tanzania, Dodoma, Sarah Jackson ambae ni mkurugenzi wa Amnesty International kanda ya Afrika Mashariki ,pembe ya Afrika na nchi za maziwa makuu, Amesema; " Hili shambulio la woga kwa mmoja wa wanasiasa washindani na maarufu linaamsha wasiwasi juu ya usalama wa sauti za wapinzani nchini (Tanzania), katika majira ambayo nafasi ya kutoa maoni inazidi kusinyaa" "Mamlaka lazima iwahakikishie Watanzania ulimwengu kwamba shambulio hili halikuhamasishwa na siasa" "Uhalifu huu usiofaa haupaswi kufagiliwa chini ya zulia, mamlaka za Tanzania lazima zianze uchunguzi makini na wa usawa mara moja kuhakikisha wale waliohusika wanashikiliwa." AWALI: Tundu Lissu, ambaye pia anaongoza chama cha wanasheria, Tanganyika Law Society, ni mkosoaji na mshamuliaji mkali wa Rais John Pombe Magufuli. Alikamatwa Julai kwa kumwita rais diktet...

JAGUAR KUACHIA WIMBO BAADA YA KUAPISHWA MBUNGE.

Mbunge wa Starehe, Kenya, "Jaguar" anajipanga kutoa wimbo mpya mara tu baada ya kuapishwa kua mbunge. Katika chapisho lake la kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii, Jaguar aliupendekeza wimbo wake wa "Ndoto" kama salamu kwa Wakenya na watu walio nje ya Kenya. Charles Njagua, ambae ni maarufu kwa jina la Jaguar, ana Aliahidi mashabiki wimbo mpya baada ya kuapa rasmi kama mbunge.  Mimbaji huyo ambaye ametoa hits kadhaa lakini sasa anazingatia siasa baada ya kushinda kiti, aliwaambia mashabiki kwenye vyombo vya habari vya kijamii kwamba wimbo mpya, unaitwa "Ndoto", uko tayari na utaachiliwa haraka baada ya kuapa. "Sasa ni karibu miongo miwili tangu mimi kuweka mguu katika studio ya kurekodi,   alisema Jaguar katika chapisho lake. CHANZO: www.tuko.news