WANAMUZIKI MAPACHA WA KUNDI LA PSQUARE, PETER (KUSHOTO) NA PAUL (KULIA) WAKIWA NA KAKA YAO AMBAE PIA NI MENEJA WAO, JUDES OKOYE. Mwanamuziki wa kundi la PSquare kutoka Nigeria, Peter Okoye ametangaza kujitoa kwenye kundi hilo la muziki wa Pop maarufu zaidi Afrika. Msanii huyo alidai kwamba amewasilisha maombi ya kuvunja kundi hilo katika barua aliyoandika kwa wakili wao Festus Keyamo. Kulingana na nakala ya barua iliyotolewa kwenye vyombo vya habari Jumatatu,Tarehe 25 Septemba, Peter alisema kuwa pacha wake na, Paul, na kaka yao, Judes waliahirisha ziara yao ya muziki ya Marekani bila kushauriana naye.Na hiyo ni moja kati ya sababu za msingi. Peter pia aliwalaumu Paul na kaka yao mkubwa mkubwa ambae ni meneja wao pia kwa udanganyifu walioufanya ili kutatua shida waliyokuwa nayo juu ya biashara ya muziki. Wasanii hao ndugu wamekua kwenye vita vya maneno kwenye mitandao ya kijamii tangu mwisho wa mwaka jana pamoja na juhudi za watu wao wa karibu kujaribu kuwapatanisha kifami...