RAISI ROBERT MUGABE. Wanasayansi wanaoheshimika kutoka chuo kikuu cha Taifa cha sayansi na teknolojia cha nchini Zimbabwe wamekua wakiendesha utafiti kwa miaka mingi kuchunguza kwanini Raisi Robert Mugabe wa nchi hiyo mwenye umri wa miaka 92 hafariki. Hii ilianza tangu mwaka 1999 ambapo iliwekwa wazi kwamba raisi huyo alikua hajawahi kubadilika sura wala nywele tangu alipoanza kutawala nchi hiyo mwaka 1980. Raisi Mugabe aliwahi kusikika akisema kwamba haitaji kwenda Gym wala kula mboga za majani ili abaki kua na afya njema sababu alizaliwa ili aishi milele. Baadhi ya watu walianza kuamini maneno hayo baada ya kuanza kuchunguza picha za raisi huyo na kugundua kwamba hana muonekano tofauti tangu miaka ya sabini mpaka sasa. Mabilioni ya dola za Kizimbabwe yaliwekezwa katika utafiti huo ambao mwisho umekuja na matokeo kwamba wataalamu hao hawakuona mvunjiko (decay) yoyote katika DNA ya raisi huyo mzee zaidi Afrika. Watafiti hao wali