Wakili wa mshtakiwa Harbinder Sethi, Joseph Makandege ameulalamikia upande wa Jamhuri kwa kushindwa kumpeleka mteja wake Hospitali ya Taifa Muhimbili kama Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilivyoamuru. Amedai hali hiyo inahatarisha afya ya mteja wake kwani akikosa kupata matibabu sahihi anaweza kupoteza maisha kutokana upasuaji aliofanyiwa uliosababisha kuwekewa maputo tumboni. “Mara mbili mahakama ilitoa amri ikielekeza utawala wa Magereza kumpeleka mshtakiwa wa kwanza Muhimbili , amri ilitolewa baada ya mahakama kukubaliana na hoja za upande wa utetezi, lakini badala ya kumpeleka Muhimbili, Magereza walimpeleka mshtakiwa Hospitali ya Amana. “Kwa taarifa za kitabibu ni kwamba hali ya mshtakiwa wa kwanza isipohudumiwa ipaswavyo inaweza kusababisha kifo kwani maputo yanaweza kupasuka tumboni , mahakama iliekeza mshtakiwa apelekwe moja kwa moja Muhimbili ambayo ni hospitali ya juu kabisa ya Serikali, ndio nategemea inaweza kuwa na wataalamu na vifaa thabiti kwa ajili ya matatizo y