Ilichapishwa Julai 29, 2017 9:36 asubuhi Seneta na bondia mashuhuri wa Ufilipino ,Manny Pacquiao, aliwasili katika eneo la vita la Marawi City Jumamosi asubuhi ili kuwatia moyo na kuwafariji askari wa nchi hiyo ambao wako vitani. Benjie Liwanag wa DzBB, akiripoti kutoka Marawi, alisema kuwa Seneta Manny Pacquiao aliwasili eneo la vita saa 9 a.m. na kukaribishwa na viongozi wa kijeshi. Kwa mujibu wa ripoti, askari walimsindikiza seneta kwenye chumba cha mkutano wa Task Force Marawi, ambapo alipewa taarifa juu ya vita katika jiji ambalo limekuwa kwenye mapigano tangu Mei 23. Baada ya mkutano huo, seneta Pacquiao ambaye nae ni askari wa akiba wa jeshi hilo la Ufilipino (reserve soldier), alifanya majadiliano na askari wanaopigana na magaidi wa Maute-ISIS ili kuwajengea molali na ujasili kisaikolojia. Pia ripoti hiyo imesema kuwa Pacquiao alitoa bidhaa za misaada kwa askari na kutumia muda mfupi wa nafasi ya kupiga picha pamoja nao. -LBG, Habari za GMA CH