DULHA SINGH. |
Dulha Singh ni kijana wa ki-Punjabi aliyezaliwa na kipande cha nywele kwenye mgongo wa chini.
Mtoto huyo alizaliwa na kipande cha nywele kwenye mgongo wake wa chini lakini familia yake ikapata hofu ya kukikata sababu inaweza kuleta bahati mbaya.
"Mama yake mara moja aliamua kukata mkia lakini alikufa kabla ya kufanya hivyo," mjomba wa Dulha Sahib Singh alisema.
"Tangu wakati huo ninamtunza Dulha na tukaamua kutokukata mkia."
Shangazi yake, Majeer Kaur, alisema watu wanasafiri kutoka mbali na kumtembelea mtoto huyo.
DULHA AKIWA NA MJOMBA NA SHANGAZI WANAEMLEA. |
"Wakati Dulha alipokuwa akiishi na mama yake, watu walitembea mamia ya maili kutafuta baraka kwa kugusa mkia wake," Bibi Kaur aliiambia The Sun."
Kwa Dulha, yeye pia anaamini mkia wake ni zawadi kutoka kwa mungu.
"Watu wanakuja kuniona kila siku. Wanataka baraka zangu. Sijui sababu lakini wanafikiri ni kama Hanuman Ji" (aina ya mzimu).
"Nadhani kuondosha mkia hautafanya vizuri mimi na familia yangu. Ni zawadi ya Mungu na sitauondoa."
"Sijisikia mbaya kuhusu kuwa na mkia. Ikiwa ni kutoka kwa Mungu, basi iwe iwe. Watu wananiheshimu kwa kuwa na mkia. "
Upendo wake wa kukwea miti unaoongezeka kila siku unawafanya watu wamtambue kama Mungu tumbili.
CHANZO :
https://au.news.yahoo.com/a/36427344/indian-boy-worshipped-as-monkey-god-after-growing-hairy-tail/#page1
Comments
Post a Comment