Kibibi kimoja cha miaka 59 katika jiji la Leicestershire,Uingereza , kimeushangaza ulimwengu baada ya kujichora tatoo zaidi ya ishirini za meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Morinho.
Bibi huyo anayeitwa Vivien Bodycote anasema kwamba yeye ni shabiki mkubwa wa Jose Mourinho na anaweza hata kumsaliti mume wake kimapenzi kwa Jose Morinho.
VIVIEN AKIONESHA TATTOO ZA KIFUANI. |
"He is not just the special one ,He is the only one" -
Alisema Vivien akimaanisha kwa katika lugha ya kiswahili kwamba Jose sio tu ni mtu maalum bali ni wa pekee pia.
Vivien ambaye ana mume wa miaka 76 anadai kwamba hawezi kwenda mjini na kurudi bila kuchora tattoo ya Mourinho na mpaka sasa ameshatumia zaidi ya pauni za Uingereza mia nane (£800) kuchora tattoo hizo.
Pia Vivien alibainisha kwamba yeye ni shabiki Manchester United kwasababu ya Morinho tu ! , na kama Mourinho atahama kwenda kufundisha nje ya Uingereza basi ndio utakua mwisho wake kushabikia timu za Uingereza!.
Bibi huyo mwenye wajukuu wanne alisema ,
" Siku niliyoambiwa na wajukuu wangu kwamba Mourinho amefukuzwa Chelsea niliwaambia Christmas ndio imeishia hapa na hakuna chakula cha jioni"
Vivien hajawai kwenda kuangalia soka uwanjani tangu miaka ya tisini lakini anasema haiwezi kupita siku bila kuangalia picha za Mourinho.
VIVIEN AKIWA NA PICHA YA MOURINHO. |
Mume wake Vivien anaitwa Tony amedai hana tatizo na ushabiki huo uliopindukia wa mke wake na kwamba yeye ndiye humwendesha kumpeleka kuchora na yeye mwenyewe ndio humlipia.
VIVIEN AKICHORA TATTOO MPYA HIVI KARIBUNI. |
VYANZO:
http://www.mirror.co.uk/sport/football/news/im-addicted-jose-mourinho-gran-10733638?ICID=FB_mirror_MF
Comments
Post a Comment