Anaandika kaka George Mwakalinga (Mtanzania anayeishi UK).
___________________________
Ukisoma magazeti ya Waingereza kuhusu ziara ya Everton, unaishia kushangaa tu na kusikitika.
(Yameandika kuhusu joto kali uwanja wa ndege). Hivi hao viongozi wote wa serikali na viongozi wa uwanja wa ndege, kweli tumeshindwa kupambana na joto la hapo ndani ya uwanja? Mbona AC bei rahisi sana? Vitu kama joto ni vitu vidogo sana wala sio vya kumsumbua mtendaji yeyote hasa kwa uwanja muhimu kama huo.
Tatizo organisation ni mbovu mno. Abiria wanavyotoka kwenye ndege na kuingia uwanjani inakuwa joto sana na foleni ndefu. Dakika 30 za kukaa hapo ni kama unachomwa moto. Vitu kama uchafu kwenye uwanja muhimu kama huo, mbona watu wengi mitaani hawana kazi? Uwanja mkuu wa nchi utakuwaje mchafu bana? Wanatutia aibu wote.
Eti dereva wa gari la Everton alivaa t-shirt ya Man united ikiwa na jina la Rooney. Unajua kutokuheshimu mambo haya madogo madogo ndio kunamtofautisha mtu mwenye uwezo na mbabaishaji. Unaipokea Everton unavaa t-shirt ya Man United. Hata kiongozi wa maandalizi hakuona shida?
Uhamiaji wenyewe shida tu wanakimbia huku na kule huku wageni wamejazana kwenye foleni.
Gari lao limetumia masaa mawili kutoka airport mpaka hotelini wakati ni umbali wa kilomita 10 tu. Ni hiyo hiyo organisation mbovu. Timu ikachelewa mpaka kwenda uwanja wa taifa kufanya mazoezi.
Magazeti ya michezo Uingereza yameandika kuwa first impression ya Everton kwa Tanzania ni kelele, kelele, kelele. Kila sehemu ni kelele kuanzia watu, magari na honi zake mpaka pikipiki.
Timu hizi kubwa zina washabiki wake ambao huwa wanazunguka nazo na ni faida kubwa kwenye utalii na hasa kuitangaza nchi.
Inatakiwa wahusika wawe wanajipanga maana ukifanya PR mbovu utakmbiza watu badala ya kuvutia watu.
Kupanga vizuri ziara kama hii haihitaji PhD ya nuclear bali uzoefu na exposure ndogo tu.!
VYANZO:
https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=1444134765678211&id=100002451047207
Comments
Post a Comment