Skip to main content

MAUAJI YA WATU WENYE VIPARA MSUMBIJI.


           Wakaazi wanaoshi katika wilaya ya kati ya Milange nchini Msumbiji wanasema kuwa miili ya watu watano wenye vipara imefukuliwa katika kipindi cha miezi mitatu kutokana na maswala ya uchawi.
Watu wanaamini kwamba mwili wa mtu mwenye kipara una dhahabu , kulingana na kamanda mmoja wa polisi kwa jina Afonso Dias alieambia BBC mnamo mwezi Juni baada ya misururu ya muaji iliolenga watu wenye vipara.
Wakaazi wa Milange wameitaka serikali kuingilia kati.
Kufikia sasa wakaazi ,na watumiaji wa dawa za kitamaduni pamoja na waliopigania uhuru wamekutana na maafisa wa taasisi ya kitaifa ya urithi na usaidizi wa haki IPAJ.
Mwakilishi wa IPAJ Antonio Gussi aliahidi kuwasilisha malalamishi yao kwa mamlaka husika ,lakini pia akawataka kutokubali tamaduni hizo zilizopitwa na wakati katika siku za usoni.

CHANZO:

Comments

Habari Nyingine Kutoka Kioo17 Swahili;

ORODHA YA NCHI 80 AMBAZO MTANZANIA ANARUHUSIWA KUINGIA BILA VIZA.

         Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza . Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza za kusafiria kama ilivyokuwa nchi za afrika Mashariki. Mhandisi Massauni amebainisha hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo kupitia tiketi ya CCM Rashid Shangazi aliyetaka kujua ni nchi ngapi ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza (viza on arrival). "Zipo nchi 16 kwa Afrika ambazo watanzania wanaweza kuzitembelea bila ya kuwa na viza na duniani zipo 67" alisema Masauni. Aidha Massauni amezitaja nchi hizo kuwa ni Benin, Burkina Faso, Cape Verde, Ivory Coast, Djibouti, Gabon, Gambia, Guinea, Guinea­Bissau, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Sierra Leone pamoja na Togo. Pamoja na hayo Masauni amesema...

MCHEZAJI WA ZAMANI WA UINGEREZA AMESEMA ALICHEZA NA WACHEZAJI WATATU MASHOGA KWENYE TIMU.

Carl Hoefkens (jezi no.2) alichezea West Bromwich Albion na Stoke City wakati wa enzi zake ligi kuu ya England. Beki wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza amesema alicheza pamoja na wachezaji wenzake wawili wa mashoga ndani ya timu, na mmoja alikua na jina kubwa. Carl Hoefkens, West Bromwich Albion na Stoke City siku za nyuma, anasema wachezaji hao walikua wazi na hawakujificha kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ingawa bado hawajulikani kwasababu ya maombi yao wenyewe ya kuomba kutotangazwa. Justin Fashanu, ambaye alijiua mwaka 1998, alikuwa mchezaji wa mwisho wa kazi nchini England kuja nje kama mashoga - mwaka 1990. Hoefkens alipokua (kushoto), alipokua anachezea Stock  City. Hoefkens aliyecheza Uingereza kwa miaka minne, akiondoka mwaka 2009, alidai kuwa mchezaji mwenzake mmoja wa timu alikua anaweza kuja kwenye uwanja wa mafunzo ya klabu na mpenzi wake wa kiume  lakini aliwaomba wenzake kutokuwaambia watu wangine wa nje ya timu. 'Nilicheza pamoja n...

MOHAMMED DEWJI NA BILL GATES KUTOA NUSU YA UTAJIRI WAO...!!!

MOHAMMED DEWJI AKIWA NA BILL GATES. Mfanyabiashara tajiri namba moja Tanzania (kwa mujibu wa jarida la Forbes) na mmiliki wa makampuni ya METL , Mohammed "Mo" Dewji ,wiki chache zilizopita amekua mmoja wa mabilionea 14 wapya kujiunga katika mpango wa kuchangia misaada kwa jamii uitwao "Giving Pledge".                 Mpango huo ulioanzishwa na familia ya mfanyabiashara tajiri namba moja duniani (kwa mujibu wa jarida la Forbes) na mmiliki wa kampuni ya Microsoft Bill Gates pamoja na rafiki yake bilionea Warren Buffet mwaka 2010, ulikua na tayari umeshaungwa mkono na mabilionea 154 mpaka mwanzo wa mwaka huu (2017). WAASISI WA "GIVIN PLEDGE",WARREN BUFFET, MELINDA GATES NA BILL GATES.         Mohammed Dewji anakua mmoja kati ya matajiri wachache sana kutoka Afrika kama Patrice Motsepe (Afrika Kusini) na Mo Ibrahim (Sudan) kujiunga na kampeni hiyo ambayo nia yake kubwa ni kushawishi watu matajiri kutoa angalau nu...

RAISI MUGABE HATAKUFA...!!!

    RAISI ROBERT MUGABE.    Wanasayansi wanaoheshimika kutoka chuo kikuu cha Taifa cha sayansi na teknolojia cha nchini Zimbabwe wamekua wakiendesha utafiti kwa miaka mingi kuchunguza kwanini Raisi Robert Mugabe wa nchi hiyo mwenye umri wa miaka 92 hafariki.    Hii ilianza tangu mwaka 1999 ambapo iliwekwa wazi kwamba raisi huyo alikua hajawahi kubadilika sura wala nywele tangu alipoanza kutawala nchi hiyo mwaka 1980.        Raisi Mugabe aliwahi kusikika akisema kwamba haitaji kwenda Gym wala kula mboga za majani ili abaki kua na afya njema sababu alizaliwa ili aishi milele.         Baadhi ya watu walianza kuamini maneno hayo baada ya kuanza kuchunguza picha za raisi huyo na kugundua kwamba hana muonekano tofauti tangu miaka ya sabini mpaka sasa.          Mabilioni ya dola za Kizimbabwe yaliwekezwa katika utafiti huo ambao mwisho umekuja na matokeo kwamba wataalamu hao hawakuona m...

MADAI YA CUBA KWAMBA WAZIRI MKUU WA CANADA NI MTOTO WA FIDEL CASTRO.

Pichani ni waziri mkuu wa Canada, Justin Trudeau (kushoto), na Rais wa zamani wa Cuba, Hayati Fidel Castro (kulia). Maelezo yaliyoandikwa na mtoto wa kwanza wa rais wa zamani wa Cuba , Fidel Castro, kabla ya kujiua yamelishtua taifa la Cuba wiki hii. Maelezo hayo yaliyoandikwa na mtoto huyo mkubwa wa mwanamapinduzi na rais wa zamani wa nchi hiyo yalikuwa ya kushangaza baada ya  kuwa na madai ya kuwa Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau ni mtoto wa nje wa baba yake marehemu Fidel Castro. Maelezo hayo yaliyoandikwa kwa mkono na mtoto huyo wa Fidel Castro aliyejiua siku chache zilizopita kwa msongo wa mawazo, Fidel Castro Diaz-Balart, aliyekuwa na umri wa miaka 68, yalionekana kuthibitisha uvumi wa muda mrefu nchini Cuba kwamba Fidel Castro ni baba wa damu wa waziri mkuu wa sasa wa Canada, Justin Trudeau ikiwa ni matokeo ya uhusiano wa siri wa kimapenzi na mke wa mwanasiasa maarufu wa Canada, Pierre Trudeau, Margaret Trudeau mwaka 1970. Kifo cha mwanasayansi wa ...

JAGUAR KUACHIA WIMBO BAADA YA KUAPISHWA MBUNGE.

Mbunge wa Starehe, Kenya, "Jaguar" anajipanga kutoa wimbo mpya mara tu baada ya kuapishwa kua mbunge. Katika chapisho lake la kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii, Jaguar aliupendekeza wimbo wake wa "Ndoto" kama salamu kwa Wakenya na watu walio nje ya Kenya. Charles Njagua, ambae ni maarufu kwa jina la Jaguar, ana Aliahidi mashabiki wimbo mpya baada ya kuapa rasmi kama mbunge.  Mimbaji huyo ambaye ametoa hits kadhaa lakini sasa anazingatia siasa baada ya kushinda kiti, aliwaambia mashabiki kwenye vyombo vya habari vya kijamii kwamba wimbo mpya, unaitwa "Ndoto", uko tayari na utaachiliwa haraka baada ya kuapa. "Sasa ni karibu miongo miwili tangu mimi kuweka mguu katika studio ya kurekodi,   alisema Jaguar katika chapisho lake. CHANZO: www.tuko.news

WAZIRI GEORGE SIMBACHAWENE AJIUZULU.

Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene ametangaza kujiuzulu nafasi yake kutokana na kutajwa kwenye ripoti za uchunguzi wa tanzanite na almasi. Akiwasilisha ripoti yake kwa Waziri Mkuu Bungeni Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Bunge iliyoundwa kuchunguza biashara ya madini ya tanzanite, Dotto Biteko, alisema Simbachawene aulizwe ni kwa nini alitoa uhamisho wa hisa za Sky Associate bila kuhusisha wataalamu kwa sababu kamati ilishindwa kuelewa ni kwa nini alifanya hivyo. “Kwa muktadha huo, ridhaa iliyotolewa Januari 30, mwaka 2015 na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo, George Simbachawene, ina dosari za kisheria na ukiukwaji wa kiutendaji na utoaji wa ridhaa hii, unainyima Stamico kipaumbele cha kununua Kampuni ya TML. “Kwa msingi huo, kamati imebaini dosari zilizofanywa za kubadilisha watoa maamuzi wa Kampuni ya TLM, zilifanyiwa kazi katika ngazi ya Wizara ya Nishati na Madini chini ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Kamishna wa Nishati na Madini na idara za sher...