Skip to main content

"BUREAU DE CHANGE" ZOTE TANZANIA KUFUTIWA LESENI.





BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa waraka kwa wafanyabiashara wa maduka ya kuuza na kununua fedha za kigeni kuomba upya leseni kwa ajili ya kufanya biashara hiyo. Leseni zote za maduka ya kubadilisha fedha za kigeni zitafutwa ifikapo Septemba 2, mwaka huu ili wamiliki waombe upya.

Hayo yalisemwa jana na Ofisa Msimamizi Maduka ya Kuuza na Kununua Fedha za Kigeni wa Benki Kuu ya Tanzania, Kanuti Mosha kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke jijini Dar es Salaam.

Mosha alisema kwa sheria ya sasa, mfanyabiashara atatakiwa kumiliki duka moja tu tofauti na ilivyokuwa awali mtu mmoja anaweza kumiliki maduka hata matano. Alisema sambamba na kutoa leseni upya, BoT imeweka viwango vipya vya mtaji ambavyo vinaanzia Sh milioni 100 hadi 300 kwa daraja A, na kuanzia Sh milioni 250 hadi Sh bilioni moja kwa daraja B na Amana ya Thamani kuanzia Dola za Marekani milioni 50 hadi milioni 100.

Aidha, alisema wafanyabiashara wa Daraja B watafanya miamala ya papo kwa hapo pamoja na miamala ya nje ya nchi. Hata hivyo, Mosha alisema mbali na masharti ya mtaji, watahitajika pia kufunga kamera tatu ‘CCTV‘ kwa ajili ya usalama.

Alieleza kuwa lengo ni kudhibiti ubadilishaji wa fedha na utoaji wa stakabadhi, kamera zinatakiwa kufungwa kaunta, kwenye kabati la kuhifadhia fedha na eneo la kuhudumia wateja.

Alisema watakaokamilisha masharti hayo ndio watakuwa wanaendesha biashara hiyo kuanzia Septemba mwaka huu Wafanyabiashara hao wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni wamepewa miezi mitatu kuanzia Juni 2, 2017 hadi Septemba mosi, mwaka huu wakamilishe usajili na kumiliki duka moja tu. Mosha alisema endapo mfanyabiashara atataka kufungua tawi, itamlazimu kutuma maombi BoT.

Comments

Habari Nyingine Kutoka Kioo17 Swahili;

MCHEZAJI WA ZAMANI WA UINGEREZA AMESEMA ALICHEZA NA WACHEZAJI WATATU MASHOGA KWENYE TIMU.

Carl Hoefkens (jezi no.2) alichezea West Bromwich Albion na Stoke City wakati wa enzi zake ligi kuu ya England. Beki wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza amesema alicheza pamoja na wachezaji wenzake wawili wa mashoga ndani ya timu, na mmoja alikua na jina kubwa. Carl Hoefkens, West Bromwich Albion na Stoke City siku za nyuma, anasema wachezaji hao walikua wazi na hawakujificha kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ingawa bado hawajulikani kwasababu ya maombi yao wenyewe ya kuomba kutotangazwa. Justin Fashanu, ambaye alijiua mwaka 1998, alikuwa mchezaji wa mwisho wa kazi nchini England kuja nje kama mashoga - mwaka 1990. Hoefkens alipokua (kushoto), alipokua anachezea Stock  City. Hoefkens aliyecheza Uingereza kwa miaka minne, akiondoka mwaka 2009, alidai kuwa mchezaji mwenzake mmoja wa timu alikua anaweza kuja kwenye uwanja wa mafunzo ya klabu na mpenzi wake wa kiume  lakini aliwaomba wenzake kutokuwaambia watu wangine wa nje ya timu. 'Nilicheza pamoja n...

STAR TV YAFUNGIWA NA TRA KWA KUKWEPA KODI.

Mamlaka ya mapato Tanzania inadaiwa kuifungia Radio Free Africa ya Mwanza inayomilikiwa na Antony Dialo kutokana na kudaiwa kodi kubwa. TRA wamewaondoa studio wafanyakazi wote na kuifunga radio hiyo. Kwa sasa ukiwasha radio utasikia matangazo ya kiingereza ya BBC. Diallo ni mwenyekiti wa CCM Mwanza na anadaiwa mamilioni ya kodi na TRA miaka mingi. Star Tv pia imekumbwa na sekeseke hilo. Ikumbukwe hii ndio TV pekee binafsi iliyokuwa ikipingana na MOAT na TEF katika sakata la RC Paul Makonda na walirusha kipindi maalum cha Makonda huku Jumuiya ya Wanahabari wakitangaza rasmi kujitenga na maswahibu yoyote yatakayokuja kuikuta RFA na Star TV. VYANZO : https://www.jamiiforums.com/threads/tra-waifungia-rfa-kwa-kudaiwa-kodi-ya-sh-bilioni-4-5.1283386/

JINSI YA KUOMBA PASSPORT YA TANZANIA KWA NJIA YA INTERNET.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia i dara ya Uhamiaji  imezindua huduma ya ujazaji fomu za maombi ya hati ya kusafiria (Passport) kwa njia ya mtandao, ambapo mwombaji atalazimika kujaza fomu hizo na kuzichapisha kabla ya kuziwasilisha kwenye ofisi za uhamiaji. Idara hiyo pia imeeleza kuwa matumizi ya huduma hiyo yataenda sambamba na huduma inayotumiwa sasa ya fomu za maombi ya pasipoti mpaka pale itakapotangazwa vinginevyo. Huduma hiyo itaanza kufanya kazi kuanzia Jumatatu tarehe  7/8/2017    na unaweza  kujaza fomu hizo  kwa kufungua tovuti hiyo ambayo ni  https://www.immigration.go.tz/ppt_application/ Utaratibu wa namna ya kujaza fomu hizo umeelekezwa katika fomu husika mtandaoni, na pia wateja wanaweza kupata ufafanuzi au maelezo zaidi kuhusu huduma hiyo kupitia anuani ya Idara ya Uhamiaji ambayo ni   info@immigration.go.tz   au katika Ofisi yoyote ya Uhamiaji iliyo karibu yako. CHANZO: http://dibute.com/muhimu-...

TUPAC SHAKUR ALIBAKWA JELA !!!

             Ulimwengu wa filamu za Hollywood na muziki wa Hip Hop juzi ulipatwa na mshangao baada ya mtayarishaji wa filamu inayohusu maisha ya hayati Tupac Shakur ,L.T Hutton kuelezea sababu zilizomfanya kumbadilisha muongozaji wa filamu hiyo kutoka John Singleton na kumuweka muongozaji Benny "Boom" Douglas.  Filamu hiyo inayoitwa "all eyez on me" tayari imekwisha andaliwa na inatarajiwa kuzinduliwa leo tarehe 16 Juni 2017.       Akizungumza kwenye mahojiano redioni L.T Hutton amewashtusha watu wengi baada ya kudai kwamba walishindwana na muongozaji wa mwanzo bwana John Singleton sababu muongozaji huyo aling'ang'ania kuwepo kwa matukio (scene) ambazo kwa maoni yake zisingependeza.        Matukio ambayo John Singleton alipenda yawepo katika filamu hiyo ni pamoja na kutaka filamu hiyo ianze na scene ya Tupac akilazimisha kumlawiti msichana wa kizungu.!!!          Singleton pia ali...

MOURINHO KUMUONDOA MKHITARYAN ILI AWEZE KUMSAJILI OZIL.

Henrikh Mkhitaryan atatupwa kando na meneja wa Manchester United Jose Mourinho ili apate nafasi ya kumsajili jiungo wa Arsenal, Mesut Ozil, kulingana na taarifa.  Bosi huyo wa Manchester United anajua lazima apunguze kikosi chake kama atataka kumsajili Ozil kutokana na madai ya mshahara mkubwa ya bingwa huyo wa Kombe la Dunia. Kiungo huyo mchezeshaji huyo ambaye mkataba wake Arsenal umalizika mwishoni mwa msimu huu, amekuwa akiomba mshahala wa Pauni Laki Tatu (£ 300,000) kwa wiki ili kukubali mkataba mpya wa kuendelea kuchezea Arsenal. Gazeti la 'The Mirror' la Uingereza limeripoti kwamba Mourinho ameamua Mkhitaryan, ambaye alijiunga na klabu kutoka Borussia Dortmund mwaka 2016, anaweza kuwa mchezaji kuondoka Ni uchaguzi wa mantiki kulingana na hali ya sasa ya mchezaji huyo katika kikosi cha Manchester United. Mchezaji huyo kutoka Armenia ameachwa mechi nane za mwisho na Mourinho huku akisema kuwa haamini kama kiungo huyo anastahilo kukukaa katika...

ORODHA YA NCHI 80 AMBAZO MTANZANIA ANARUHUSIWA KUINGIA BILA VIZA.

         Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza . Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza za kusafiria kama ilivyokuwa nchi za afrika Mashariki. Mhandisi Massauni amebainisha hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo kupitia tiketi ya CCM Rashid Shangazi aliyetaka kujua ni nchi ngapi ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza (viza on arrival). "Zipo nchi 16 kwa Afrika ambazo watanzania wanaweza kuzitembelea bila ya kuwa na viza na duniani zipo 67" alisema Masauni. Aidha Massauni amezitaja nchi hizo kuwa ni Benin, Burkina Faso, Cape Verde, Ivory Coast, Djibouti, Gabon, Gambia, Guinea, Guinea­Bissau, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Sierra Leone pamoja na Togo. Pamoja na hayo Masauni amesema...