Na BERNADINE MUTANU Imepakiwa - Wednesday, August 16 2017 at 11:11 Kwa Mukhtasari VISA vya dosari kwenye uchaguzi uliokamilika vinazidi kuripotiwa nchini Kenya, wiki moja baada ya wananchi kupiga kura, na siku kadhaa baada ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kutangaza mshindi wa urais. Huku IEBC ikikosolewa kwa kutangaza matokeo ya mwisho ya urais Ijumaa usiku kabla ya matokeo yote kuingia, imeibuka kuwa kituo kimoja Kaunti ya Mandera kilitumia karatasi ya kawaida kurekodi matokeo ya urais, badala ya kutumia Fomu 34 A. Matokeo hayo yaliwekwa katika tovuti ya IEBC, na kushangaza wananchi, huku madai ya wizi wa kura yakizidi kuchacha. 'Fomu’ hiyo isiyo ya kawaida iliwekwa katika mtandao wa IEBC kutoka Kituo cha Kuhesabia kura cha Bulla Dadacha 2, Wadi ya Elwak Kusini, Eneo Bunge la Mandera Kusini, Kaunti ya Mandera. Haina nambari ya mfuatano (serial number) kama fomu za kawaida za uchaguzi,...


Comments
Post a Comment