Skip to main content

MAJIBU YA FREDRICK WEREMA KUHUSU KUMUITA KAFULILA "TUMBILI".


FREDRICK WEREMA.



               Dar es Salaam. Mjadala mkali wa sakata la uchotwaji fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow ulisababisha aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, Jaji Fredrick Werema kutumia msemo unaomtaja tumbili wakati akimjibu mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini, David Kafulila.
Werema alijitokeza jana kufafanua kuhusu kauli yake, lakini mjadala huo wakati huo ulikuwa na matamko tofauti wakati joto bungeni lilipozidi, likigawa wabunge na hata viongozi wa Serikali.
Katika hotuba yake akiwa jimbo la Kigoma Kusini juzi, Rais John Magufuli alifufua tena mjadala huo wakati alipompongeza “kwa dhati” Kafulila kwa uzalendo wake wa kuibua kashfa hiyo iliyohusu Sh306 bilioni na kusimamia kutetea hoja yake hadi mwisho.
Rais alisema Kafulila alipata shida hadi baadhi walimuita tumbili, neno lililotamkwa na Werema wakati akijibu mwongozo wa mbunge huyo wa Kigoma Kusini, na kwamba waliomuita hivyo sasa wamegeuka tumbili.
“Lazima niwe mkweli na nisiposema hapa nitakuwa sijaitendea haki nafsi yangu, siku zote ukweli utabaki kuwa ukweli tu na ndiyo maana nampongeza Kafulila kwa sababu alisimama imara kupigania maslahi ya umma. Alionyesha uzalendo wa hali ya juu unaopaswa kuigwa na kila mmoja wetu,” alisema Rais.
Jana, Werema alimwambia mwandishi wetu kuwa alisema neno hilo kama msemo wa Kiswahili. Mwandishi wetu alipomuuliza kuhusu kauli ya Rais juzi, Jaji Werema alijibu:
Jaji Werema: Sasa unataka nifanyeje?
Mwandishi: Tunahitaji maoni yako kuhusu kauli hii.
Jaji Werema: Hilo jambo si liko mahakamani? Tunaweza kushtakiwa, wako mahakamani?
Mwandishi: Sawa. Lakini kwa kipindi kile kati ya watu ambao walimuita Kafulila tumbili, wewe ni mmoja wao.
Jaji Werema: Unajua wengi walishindwa kuelewa nilisema nini, mimi nilichokizungumza ni kwamba tumbili haamui mambo ya msituni, na huo ni msemo wa kawaida tu.
Kafulila, ambaye alikuwa mbunge wa Kigoma Kusini kuanzia 2010 hadi 2015 kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, aliibua kashfa hiyo bungeni baada ya kuisoma katika gazeti la The Citizen mwaka 2014.
Kwenye sakata hilo jumla ya Sh306 bilioni zilichotwa kutoka akaunti hiyo iliyofunguliwa kwa pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kampuni ya kufua umeme ya IPTL baada ya kutokukubaliana katika tozo ya uwekezaji.
Baada ya Kafulila kuanzisha mjadala huo, Bunge liliagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi na taarifa yake ilitumiwa na chombo hicho cha kuisimamia Serikali kujadili kwa kina uchotwaji wa fedha hizo.
Licha ya kwamba wabunge wa CCM waliungana na upinzani katika sakata hilo, mjadala ulitawaliwa na mihemko na ushabiki na haikuwa ajabu kwa Werema kujikuta akitoa kauli hiyo.
Kila mbunge aliyesimama kutaka hatua zichukuliwe dhidi ya wote waliohusika, ukumbi ulikaa kimya kusikiliza lakini aliposimama mbunge aliyetetea kuwa fedha za escrow hazikuwa za umma kulikuwa na kelele za kumpinga na za kumshangilia, kiasi cha kulazimisha kiti cha spika kutuliza hali kila wakati.
Wakati Bunge lilipofikia kuweka maazimio, kikao kilifanyika hadi saa 5:00 usiku bila ya kufikia muafaka na kulazimika kuahirisha hadi siku iliyofuata kutoa nafasi kwa wabunge kujadiliana maazimio.
Miongoni mwa hoja zilizotolewa kukuza tatizo hilo ni zile zilizotolewa na mbunge wa zamani wa Nkenge (CCM), Assumpter Mshama, ambaye alidai kuna watu wengine waliopewa fedha wakiwa Mombasa nchini Kenya, na kumtaja mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuwa mmojawao.
“Hata mheshimiwa Mbowe amediriki kutajwa kwamba alipokea pesa kule Mombasa, lakini humu hakuna taarifa zake. Taarifa za benki ya Stanbic hatujasikia taarifa zake, lakini wanaojulikana wamepata pesa ni wa CCM. Ndio maana tunasema hata kama hiyo kamati ya PAC,” alisema huku sauti ikitaka kutoa taarifa.
Mshama alitakiwa atoe ushahidi kuwa Mbowe alitoa fedha lakini alishindwa na baadaye kufuta kauli yake.
Mwingine aliyetetea kuwa fedha hizo hazikuwa za Serikali ni mbunge wa Magomeni (CCM), Mohamed Chombo aliyewatuhumu walioshupalia suala hilo kuwa walikuwa na uchu wa madaraka.
“Sasa hivi, VIP imenunuliwa na PAP. Inabidi yeye-- kwa maana ya PAP-- alipe fedha zake za hisa parcent (asilimia) 30. Fedha hizi baada ya kutoka, PAP inabidi amlipe VIP. Sasa ndugu yangu nataka niwaambie--sasa nataka kuja kwenye ile ashki majinuni ni nani,” alisema.
“Kuna watu ambao maisha yao yote, wao ni watu wenye ashki. Ashki ni hamu ya kutaka na wao wapate kila wanachokipata wengine. Kuna watu wana ashki ya kupata madaraka haya.”

CHANZO ;
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Aliyemuita-Kafulila-tumbili-afafanua/1597578-4030898-g5oxnnz/index.html

Comments

Habari Nyingine Kutoka Kioo17 Swahili;

ORODHA YA NCHI 80 AMBAZO MTANZANIA ANARUHUSIWA KUINGIA BILA VIZA.

         Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza . Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza za kusafiria kama ilivyokuwa nchi za afrika Mashariki. Mhandisi Massauni amebainisha hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo kupitia tiketi ya CCM Rashid Shangazi aliyetaka kujua ni nchi ngapi ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza (viza on arrival). "Zipo nchi 16 kwa Afrika ambazo watanzania wanaweza kuzitembelea bila ya kuwa na viza na duniani zipo 67" alisema Masauni. Aidha Massauni amezitaja nchi hizo kuwa ni Benin, Burkina Faso, Cape Verde, Ivory Coast, Djibouti, Gabon, Gambia, Guinea, Guinea­Bissau, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Sierra Leone pamoja na Togo. Pamoja na hayo Masauni amesema zipo nyingine

MCHEZAJI WA ZAMANI WA UINGEREZA AMESEMA ALICHEZA NA WACHEZAJI WATATU MASHOGA KWENYE TIMU.

Carl Hoefkens (jezi no.2) alichezea West Bromwich Albion na Stoke City wakati wa enzi zake ligi kuu ya England. Beki wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza amesema alicheza pamoja na wachezaji wenzake wawili wa mashoga ndani ya timu, na mmoja alikua na jina kubwa. Carl Hoefkens, West Bromwich Albion na Stoke City siku za nyuma, anasema wachezaji hao walikua wazi na hawakujificha kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ingawa bado hawajulikani kwasababu ya maombi yao wenyewe ya kuomba kutotangazwa. Justin Fashanu, ambaye alijiua mwaka 1998, alikuwa mchezaji wa mwisho wa kazi nchini England kuja nje kama mashoga - mwaka 1990. Hoefkens alipokua (kushoto), alipokua anachezea Stock  City. Hoefkens aliyecheza Uingereza kwa miaka minne, akiondoka mwaka 2009, alidai kuwa mchezaji mwenzake mmoja wa timu alikua anaweza kuja kwenye uwanja wa mafunzo ya klabu na mpenzi wake wa kiume  lakini aliwaomba wenzake kutokuwaambia watu wangine wa nje ya timu. 'Nilicheza pamoja na was

UTATA WA FORM 34A FEKI KATIKA TOVUTI YA IEBC.

  Na BERNADINE MUTANU  Imepakiwa - Wednesday, August 16   2017 at  11:11 Kwa Mukhtasari VISA vya dosari kwenye uchaguzi uliokamilika vinazidi kuripotiwa nchini Kenya, wiki moja baada ya wananchi kupiga kura, na siku kadhaa baada ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kutangaza mshindi wa urais. Huku IEBC ikikosolewa kwa kutangaza matokeo ya mwisho ya urais Ijumaa usiku kabla ya matokeo yote kuingia, imeibuka kuwa kituo kimoja Kaunti ya Mandera kilitumia karatasi ya kawaida kurekodi matokeo ya urais, badala ya kutumia Fomu 34 A. Matokeo hayo yaliwekwa katika tovuti ya IEBC, na kushangaza wananchi, huku madai ya wizi wa kura yakizidi kuchacha. 'Fomu’ hiyo isiyo ya kawaida iliwekwa katika mtandao wa IEBC kutoka Kituo cha Kuhesabia kura cha Bulla Dadacha 2, Wadi ya Elwak Kusini, Eneo Bunge la Mandera Kusini, Kaunti ya Mandera. Haina nambari ya mfuatano  (serial number)  kama fomu za kawaida za uchaguzi, haina majina ya maajenti waliosimamia uchagu

EL HADJI DIOF KUWA MBUNGE SENEGAL.

EL HADJI DIOF (kombe la dunia 2002)        Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Senegal El Hadji Diof ametangaza nia yake ya kutaka kugombea ubunge nchini humo.      Diof ambaye alistaafu kucheza soka mwaka 2015, alisema:   "Baadae yangu inajulikana, ndani ya miaka miwili nitaingia kwenye siasa sababu najua kuanzia kwenye hatua hiyo nitaweza kubadilisha mengi kwenye soka..."  "Ninapenda siasa, nina washauri wazuri Senegal na hayo ndio maisha yangu ya baadae sababu watu wa Senegal wanaweza kunisikiliza." "Nimesoma kozi za juu kabisa za ukocha lakini nina mipango mizuri zaidi kwenye vitu ninavyotaka kufanya" "Lakini nipo tayari kuishauri timu yangu (Senegal) muda wowote nikihitajika."        El Hadji Diof alikua mchezaji tegemeo katika kikosi cha timu ya taifa ya Senegal iliyofuzu kucheza kombe la dunia kwa mara ya kwanza mwaka 2002 na kua timu ya pili ya Afrika kufika hatua ya robo fainali baada ya Cameroon mwaka 1990. Tazama k

RAPA SNOOP DOGG AMETHIBITISHA MIPANGO YA KUHAMIA UGANDA.

Msanii wa muziki wa Hip Hop wa Marekani, Calvin Cordozar Broadus.Jr. maarufu kama Snoop Dogg amethibitisha kuwa anataka kuhamia Uganda baada ya rais wa Marekani, Donald Trump kudaiwa kuziita nchi za Afrika 'Shimo la Choo' . Snoop Doggy Dogg pia ni mwimbaji, mwandishi wa nyimbo, mtayarishaji wa muziki, mtangazaji katika televisheni, na mwigizaji wa filamu ambaye alianza kupata umaarufu mkubwa katika muziki mwaka 1992 wakati alipogunduliwa na mtayarishaji Dr.Dre, na kushiriki katika nyimbo za Dr.Dre kama "Deep Cover", na kisha kwenye albamu ya kwanza ya Dr.Dre, ' The Chronic' . Kwa sasa tayari ameshauza albamu zaidi ya milioni 23 nchini Marekani na albamu milioni 35 duniani kote. Mmarekani huyo mweusi mwenye miaka 46 wa ambaye anajulikana kwa nyimbo zake za maarufu kama; The next episode, Drop it like it’s hot, beautiful, Lay low,  nk Juzi alirekodi kipande cha video na kukisambaza akisema kuwa anataka kuhamia chini Uganda. Tazama V

NAPE ASEMA KWAMBA TUNDU LISSU ALIMWAMBIA WANATAFUTWA, AHAME CCM.

MBUNGE WA MTAMA (CCM) AKICHEKA NA TUNDU LISSU MUDA MFUPI KABLA YA KUPIGWA RISASI. Imeandikwa na Edwin Mjwahuzi , Mwananchi; emjwahuzi@mwananchi.co.tz Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (kulia) akifurahia jambo na mbunge wa Mtama, Nape Nnauye walipokuwa wakitoka kuhudhuria kikao cha Bunge, mjini Dodoma jana mchana. By Edwin Mjwahuzi, Mwananchi; emjwahuzi@mwananchi.co.tz Dodoma. Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye ameeleza alichoambiwa na Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu jana Alhamisi mchana wakati wakitoka bungeni huku wakicheka. Nape amesema Lissu alimwambia, “Wewe Nape ni mjomba wangu, kwa nini unabaki CCM? Mimi na wewe tunafuatiliwa na jamaa zako wakitumia gari moja. Mimi na wewe ni watuhumiwa, hama CCM mjomba.” Lissu alipigwa risasi jana Alhamisi mchana na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na baadaye usiku alihamishiwa Hospitali ya Aga Khan ya Nairobi nchini Kenya. Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini jana wakati Lissu

ORODHA YA NCHI ZA KWANZA NA ZA MWISHO KWA AMANI DUNIANI.

Marekani:  Ripoti ya Taasisi ya Uchumi na Amani imepata mataifa kumi tu ulimwenguni ambayo hayapo katika vita na migogoro kabisa. Kwa mujibu wa Ripoti ya Kimataifa ya Amani 2016, Botswana, Chile, Costa Rica, Japan, Mauritius, Panama, Qatar, Uswisi, Uruguay na Vietnam ndio nchi pekee ambazo hazipo kwenye vita wala migogoro yeyote ile ya kuhatarisha amani.. Iceland inaongoza orodha ya nchi zinazoongoza kwa amani ulimwenguni, ikifuatiwa na Denmark, Austria, New Zealand, Ureno, Jamhuri ya Czech, Uswisi, Canada, Japan na Slovenia - wakati Marekani ikiwa kwenye nafasi ya 103. Palestina imepanda kutoka nafasi ya 163 mpaka nafasi ya 148. Syria iliyoharibiwa na vita imewekwa chini ya orodha, chini kuliko Sudan Kusini, Iraq, Afghanistan, Somalia, Yemen, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ukraine, Sudan na Libya. "Ripoti inalinganisha amani duniani kwa kutumia mandhari tatu pana: hali ya utulivu na usalama katika jamii; kiwango cha mgogoro wa ndani au wa kimataifa; na kiwango cha kije