Serikali ya Emmerson Mnangagwa inataka kutumia huduma za Interpol(Polisi wa kimataifa) kuwasaka washirika wa karibu wa rais Robert Mugabe ambao walikimbia nchi wakati jeshi lilipositisha utawala wa zamani mwezi uliopita. Mawaziri wa zamani Jonathan Moyo, Saviour Kasukuwere na Paddy Zhanda wanaaminika kuwa ndio walengwa wakuu wa msako huo kwa sababu za tuhuma za uhalifu unaohusishwa na rushwa. Tume ya kupambana na rushwa ya Zimbabwe, Zimbabwe Anti-Corruption Commission (ZACC) inachunguza tuhuma za Moyo za wizi katika Shirika la Maendeleo ya Wanawake wa Zimbabwe wakati wa utawala wa Mugabe. Moyo alidai kuwa Mnangagwa alikuwa akitumia ZACC kutekeleza visasi binafsi vinavyohusishwa na mapambano ya kutaka kumrithi Mugabe. ZACC tayari imekamata washirika wa karibu wa Mugabe yaani Joseph Made, Walter Chidakwa, Ignatius Chombo na Jason Machaya. Viongozi wa zamani wa vijana wa chama tawala cha Zanu PF, Kudzanai Chipanga na Innocent Hamandishe pia walikamatwa kwa mashtaka ya jin