Picha za zinazo onesha kasisi wa Uganda akipigwa mabusu na wafuasi wake miguuni tayari zimekwisha zua gumzo miongoni mwa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa siku za karibuni. Mtume Elvis Mbonye, mwenye umri wa miaka 40, wa Zoe Fellowship, Jumapili iliyopita aliandaa tafrija ya chakula cha jioni kwa kiingilio cha takribani dola 185 (185$) kwa tiketi za platinum, dola 210 (210$) kwa tiketi za Gold, dola 135 (135$) kwa tiketi za Silver, na dola 75 (75$) kwa tiketi za kawaida. Ibada za Mbonye hufanyika siku za Jumanne kinyume na za makanisa mangine za Jumapili au Jumamosi, akisema Mungu alimwambia afanye ibada siku za Jumanne. Wakati alipoanza kanisa mwaka 2014, Mbonye alikuwa na waumini 100, lakini sasa amefikisha waumini 5,000 , vyombo vya habari vya Uganda vinasema. Mbonye, kabla ya kuhamishia ibada zake kwenye uwanja wa Rugby wa Kyadondo, alikua anakodisha hoteli ya kifahari ya Kampala kwa gharama sawa na dola 13,500 za kimarekani kila wiki.